Jinsi binti wa miaka 17 alivyotumia Mtandao wa YouTube kujifungua mtoto peke yake

Muhtasari
  • Jinsi binti wa miaka 17 alivyotumia Mtandao wa YouTube kujifungua mtoto peke yake

Katika eneo moja huko Kerala, India, binti mdogo wa miaka 17 alijifungua mtoto wa kike peke yake bila usaidizi wa mkunga wa jadi ama wahudumu wa hospitali akisaidiwa na mtandao wa YouTube.. Baada ya kujigungua, binti huyo aliendelea kukaa ndani kwa siku tatu.

Gazeti la Hindustan Times limenukuu shirika la PTI kwamba baadae mama wa binti huyo aiyejifungua Oktoba 20, alimpeleka Hospitali.

Familia ya mvulana aliyempa ujauzito binti huyo inaendelea kumhudumia yeye na mtoto aliyezaliwa lakini Polisi wamemfungulia mashtaka ya ubakaji.

Ukweli ni kwamba familia za pande zote mbili zinataka vijana hao waoane, na walikuwa wakisubiri binti afikishe miaka 18, utaratibu rasmi ufanyike.

Kwa mujibu wa taarifa za awali ni kwamba, biti huyo aliamua kutotafuta msaada popote wakati akijifungua akitumia video za Youtube, zinazoonesha namna ya mwanamke anavyoweza kujifungua.

Sajesh Bhaskar, mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa mtoto Malapuram alisema alitaarifiwa na Hospitali alikopelekwa binti huyo kuhusu taarifa hiyo. Binti na mtoto wake kwa ujumla wako salama, wakiwa chini ya uangalizi wa mama wa binti huyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo, Polisi walimkamata akijana aliyempa ujauzito, kijana mweye umri wa miaka 21.

"Mama wa binti huyu mwenye miaka 50, hakujua kuhusu ujauzito huu wa mwanawe wala kujifungua," alisema. Baba wa mtoto ni mlinzi hivyo mara yingi usiku anakuwa lindoni na mchana huutumia kupumzika.

"Binti alijifungia chumbani na kujfungua, mama alidhani alikua kwenye 'masomo kupitia mtandao."

Kutokana na janga la Corona kwa muda wanafunzi wemekuwa wakitumia mitandao kuhudhuria masomo yao.

" YouTube ilimsaidia kujua namna gani ya kukata kondo la uzazi baada ya kujifungua".

Wataalamu wanasemaje?

Ukifuatilia mitazamo ya watalaamu kuhusu kujifungua kwa mwanamke, watalaamu wengi wanashauri mwanamke kuhudhuria Kliniki mara kwa mara.

Wengi wanaweza kujiuliza ilikuwaje binti huyu akaweza kuishi na mama yake na ndugu zake wengine wote bila kujlikana kwamba ni mja mzito mpaka akaweza kujifungua kwa kificho? lakini ushauri wa kitaalamu ni kwamba mama mjamzito ni lazima afuatiliwe afya yake na afya ya mtoto wake tumboni wakati wote kabla na baada ya kujifungua.

Mmoja wa madaktari waliochapisha kwenye mtandao wa UYL Cliniki Tanzania anasema ni muhimu mama kwenda kiliniki mapema ili

  • Kuzuia, kugundua na kutibu mambo yanayodhuru ujauzito
  • Kutoa ushauri, elimu, kuwapa uhakika na msaada mama na mtoto wake
  • Kutatua matatizo madogo madogo ya ujauzito