Hirsutism: 'Nilikuwa nikinyoa kila wiki nisionekane kama mwanamume'

Muhtasari
  • Wanaume huniita 'mwanamume' kwa ajili ya nywelie mwilini mwangu
Image: BBC

Chidube Nwaonicha-Emegha mwenye umri wa miaka 19 ameyaona mengi kuanzia akiwa na umri wa miaka 16-mara ya kwanza alipogundua kwamba anamea nywele katika sehemu ambazo mwanamke hafai kuwa na nywele.

Ukifikiri huo ulikuwa mshtuko kwake ,ngoja usikie simulizi yake kuhusu yote aliyoyapitia akiwa shuleni na hata baada yta kumaliza shule

Chidube mwenye umri wa miaka 19 sasa ana hali iitwayo Hirsutism ambayo husababisha wanawake kuwa na nywele nyeusi katika uso,kifuani,shingoni na chini-mgongoni.

Hirsutism husababishwa na matatizo kadhaa na katika hali ya Chidume imesababishwa na ugonjwa wa polycystic ovary syndrome (PCOS).

Lakini mara nyingi, hutokea bila sababu inayotambulika, na kwa ujumla haichukuliwi kuwa inaweza kuzuilika, kulingana na Kliniki ya Mayo.

Chidube anatumia mtandao wake wa kijamii kuongeza ufahamu kuhusu hali yake na kuwahimiza wengine kujivunia kuwa wa kipekee.

Anasema kabla ya kujikubali na kuikubali hali yake alilazimika sana kuepuka hata kufikiria kuhusu hali hiyo na akiwa shule ya upili anasema alihakikisha kwamba anajinyoa kila wiki.

'Nilipokuwa katika shule ya upili nilikuwa nikinyoa kila wiki na ningekuwa na alama shingoni na mamangu angeshangaa na kuniuliza mbona najisumbua kuondoa nywele hizo' anasema Chidube.

Lakini katika yote hakuna kikubwa kama kuonekana kwa njia ya kubaguliwa ama kutazamwa kama kiumbe mwenye udhaifu Fulani kwa sababu ya hali yake anasimulia jinsi kijana mmoja aliyekuwa Rafiki wake ambaye alimuita 'mwanamme'

'Nilikuwa na ugomvi na jamaa mmoja …kisha akaniita 'Mr.man' . Nilihisi vibaya na kila mtu akaanza kuniita mwanamme'

Wasichana kuachwa na wapenzi wao

Katika hilo ,hayuko peke yake kwani baada ya kuanzisha uhamasisho kuhusu hali yake na kujipata amekutana na wengi kote duniani wenye hali kama yake alisikia kuhusu mengi ambayo wasichana wenzake wenye nywele katika sehemu zisizo za kawaida kwa wanawake wanayapitia.Wengine waliachwa hat ana wapenzi wao .

Katika safari yake ya kujikubali Chidube anasema kuna wakati alikuwa hata akiwaza kuhusu iwapo atawahi kupata Watoto ama hata kukoma kuwa mkubwa Zaidi . Maswali hayo yote yalimkosesha usingizi lakini amepata Faraja baada ya kugundua kwamba hali yake haimzuii kuendelea na Maisha yake kama watu wengine wa kawaida .

'Ni kitu cha kushtua kwa sababu PCOS sio kitu unachoweza kuwa nacho kisha upuuze tu wakati mwingine huwa nakifirkia sana' anasema

Kwa Chidube kibarua sasa ni kuwepo kwa ajili ya maelfu ya wasichana kama yeye na anatumia mitandao ya kijamii kuwaunganisha na kuwawezesha kuelezea Maisha yao .

'Nilianza kukubali hali yangu baada ya kuweka picha hizi mtandaoni katika Instagram mapema mwaka huu.Nimekuwa na aibu kuhusu hali yangu .Wasichana wengi kutoka nchi mbali mbai walianza kuwasiliana nami na kunisimulia wanayopitia. '

Hali yenyewe inaanzaje?

Hirsutism ni hali ya mwanamke kuwa na kiwango cha juu cha homoni za androgen za kiume ambazo huwezesha kumea kwa nywele katika sehemu ambako nywele humea kwa wanaume kama vile kifua,usoni,mgongo na shingoni. Hali hiyo husababishwa na sababu nyingi ikiwemo polycystic Ovary syndrome(PCOS) na wakati mwingine ingawaje kwa nadra sana aina Fulani ya uvimbe .

Hali hii hutokea bila kichocheo na haiwezi kuzuilika. Kwa wanawake wanaohitaji matibabu ,lazima tatizo la mwanzo ama chanzo litibiwe

Kujiamini na mwanzo mpya

Tatizo hili la kutokewa nywele kama mwanamme halijamzima chidube na ndoto zake kwani ufahamu aliopata na simulizi ya wasichana kama yeye umempa mwelekeo mpya na ari ya kuwapigania kwa kutoa uhamasisho kupitia picha na jumbe zake katika mitandao ya kijamii .

'Sasa najiamini zaidi kwa sababu ya kufahamu kwamba kuna wasichana wengine wanaopambana na hali kama hii yangu' anasema

'Mimi ndio msichana pekee mwenye nywele nyingi wakati napojipata kwenye umati wa watu kwa hivyo najihisi kuwa spesheli.Watu wengi huniangalia na kushangaa jinsi nilivyo na nywele kama mwanamme .

Ni kitu kinachonifanya nijihisi kwa njia ya kipekee. Tunafaa kujikubali jinsi tulivyo kama wanawake..sisi ni watu spesheli sana'