Mambo muhimu ya kujifunza kutokana na mkasa wa basi Mwingi

Muhtasari

•Basi hilo ambalo lilikuwa limebeba waumini waliokuwa wanaelekea kuhudhuria harusi liliwezwa nguvu na mikondo mizito ya maji wakati lilijaribu kuvuka daraja lililokuwa limefurika maji  mida ya alasiri siku ya Jumamosi.

Basi lililozama
Basi lililozama
Image: HISANI

Siku ya Jumamosi biwi la simanzi lilitanda kote nchini baada ya basi lililokuwa limebeba zaidi ya watu 40 wakiwemo watoto kutumbukia mto Enziu katika kaunti ya Mwingi na kuua zaidi ya watu 32. Habari za mkasa huo ziliacha wengi vinywa wazi.

Basi hilo ambalo lilikuwa limebeba waumini waliokuwa wanaelekea kuhudhuria harusi lilizidiwa na mawimbi ya maji ya mto Enziu na kusombwa na maji ya mto Enziu   mida ya alasiri siku ya Jumamosi.

Maelfu ya Wakenya wameendelea kuomboleza walioangamia katika mkasa huo huku wakipata mafunzo mbalimbali ya kuzuia tukio kama hilo kutokea tena.

Lakini Je!ni mambo yepi unayofaaa kuzingatia wakati kuna mafuriko, haya hapa baadhi ya mambo ambayo yamezungumziwa zaidi:-

Dereva kumakinika zaidi:-

Madereva kote nchini wameshauriwa kuwa makini zaidi barabarani haswa katika msimu huu wa mvua.

Ajali nyingi huripotiwa msimu wa mvua kutokana na mabadiliko ya barabara na ardi yanayochangiwa na mafuriko ya maji.

Aghalabu barabara huwa telezi huku zingine zikifurika maji katika sehemu mbalimbali za nchi haswa zilizo tambarare. 

Rais Kenyatta alipokuwa anaomboleza walioangamia katika mkasa wa Mwingi alitoa tahadahari dhidi ya kujaribu kuvuka mito iliyofurika katika msimu huu wa mvua.

"Rais anapenda kuwakumbusha Wakenya kote nchini kutii ushauri wa Serikali dhidi ya kujaribu kuvuka mito iliyojaa maji hasa wakati wa msimu wa mvua" Msemaji wa ikulu Kanze Dena alisema.

Wengi wamekosoa dereva wa basilhatua ya basi lililohusika kwenye ajali kujaribu kuvuka mto Enziu ilhali ulikuwa umefurika.

Serikali kuwekeza zaidi kwenye miundombinu:-

Baadhi ya Wakenya wamenyooshea serikali kidole cha lawama kufuatia mkasa uliotokea Mwingi wakilalamikia barabara mbovu na ukosefu wa daraja bora katika eneo ambalo basi lilitumbukia majini.

Ni dhana ya wengi kwamba kungekuwa na daraja nzuri pale ajali  ile isingepatikana. 

Mkasa huo unafaa kupatia serikali shinikizo la kuboresha hali ya barabara nchini na kuhakikisha kwamba daraja zimewekwa katika maeneo yenye mito ama mabonde ambapo magari ama watu huvukia  kwani ifikapo msimu wa mvua huenda matukio kama yale yakatokea tena.

Kufuatia ajali  iliyotokea Jumamosi, gavana wa Kitui Charity Ngilu alihakikishia wakazi kwamba serikali kuu imeanzisha mpango wa kujenga daraja katika eneo la ajali ili kuzuia msiba mwingine.

Abiria kuwa na subira wakiwa safarini:-

Ripoti kadhaa zimechipuka zikisema abiria ndio walishinikiza dereva kuvuka maji yale wakati ajali ilitokea.

Ni vyema abiria kuwa na subira wakati wanaposafiri kwani kwa kawaida dereva anaelewa zaidi hali ya barabara.

Dereva anaposita kuvuka eneo fulani ni vyema kuelewa badala ya kumshinikiza kuvuka kwani huenda ana sababu nzuri za kufanya vile.

Vile vile dereva anapobadilisha kasi na kuanza kuendesha polepole haswa mida ya usiku ama wakati wa mvua  ni vyema kuelewa kwani huenda anashuhudia matatizo ambayo asipochunga  ni rahisi kusababisha ajali.