Kutana na msichana wa umri wa miaka 9 fundi wa pikipiki

Muhtasari
  • Kutana na msichana wa umri wa miaka 9 fundi wa pikipiki
Image: BBC

Watoto wengi walio umri sawa na wake hulilia asikrimu, wengine hutumia muda wao kutazama katuni na wengine kucheza nje lakini kwa Susanna Adjakie Apekor kwake mambo ni tofauti.

Susanna sasa amekuwa mtaalamu wa kukarabati pikipiki, akizungumza na BBC Pidgin anasema kwa umri wake anaweza kumfunza yeyote jinsi ya kukarabati pikipiki.

Ilikuwaje akavutiwa na pikipiki?

Susanna anasema akiwa na umri wa miaka mitatu, baba yake alienda kuwatembelea yeye na mama yake na mara nyingi angesimulia vile alikuwa na kazi nyingi.

Kwa hivyo siku moja akamueleza kuwa yeye alikuwa ni fundi wa kukarabati pikipiki.

ili naye apate kijifunza kukarabati pikipiki.

Na mama yake akapenda wazo hilo na kuhamia eneo baba yake alikuwa akifanyia kazi ili aweze kupata muda zaidi wa kujifunza

Wakati baba yeka, Awudu alipozungumza na BBC Pidgin alisema licha ya kuwa bado hajafikia kiwango cha kuimarika kabisa kasi aliojifunza nayo imewashangaza.

 

Baada ya muda mfupi alikuwa tayari ameelewa mambo kadhaa kwenye duka, kitu ambacho si cha kawaida kwa umri wake.

Laki kwa sababu alikuwa akiendelea vyema mama yake alimruhusu aendelee kujifunza.

Kulingana na Awudu, kwa sasa hakuna hitilafu ya pikipiki ambayo Susanna atashindwa kuirekebisha.

Anachanganya vipi Shule na ufundi wa pikipiki?

Mchana Susanna uhudhuria masomo kama watoto wengine.

Kwa sasa anasoma darasa la tatu.

Akiongea na BBC Pidgin Susanna anasema anapotoka shuleni yeye hubadilisha mavazi na kwenda kazini.

"Pale baba yangu huendelea kunifunza jinsi ya kukarabati pikipiki," anasema.

Kwa miaka kadhaa amejifunza kurekebisha injini, breki, nyororo na mambo mengine kadhaa.

Wanafunzi wenzangu huniambia watanisaidia siku moja

Kinyume na watoto wengi shuleni, watoto wa rika lake tayari wana ujuzi wa kukarabati pikipiki.

Wanasema mimi si kawaida na hunishauri niendelea kujifunza zaidi na ukarabati wa pikipiki.

"Wanafunzi wenzangu huniambia niendeleeā€¦ huenda ikanisadia siku moja" anasema.

 

Ninataka kujifunza kukarabati ndege

Susanna ana mpango kwa siku za usoni ambao ana lengo la kumiliki duka lake ambapo atafanya kazi kama mekanika.

Lakini hii ni moja ya ndoto zake, anasema lengo lake ni kukarabati ndege.

 

"Nikikuwa mkubwa ninataka kujifunza kurekebisha ndege, magari na boti" anasema.