Kisiwa ambacho wanaume hutengeneza miili yao ionekane kama ngozi ya mamba

Wanyama wanaowaheshimu sana ni pamoja na tai, nguruwe, nyoka na mamba.

Image: BBC

Nchini Papua New Guinea, 80% ya wakazi wanaoishi katika vijiji vya pembezoni, ambavyo vingi vipo katika sehemu za mbali za nchi na hawana mawasiliano ya karibu na maeneo mengine duniani.

Mwandishi wa habari hii aligundua kuwa watu wa jamii hii bado wanafuata mila na desturi za zamani.

Wanaume katika nchi hiyo huweka alama tofauti, kila moja ikiwa na maana yake, ili kutimiza desturi za kale za mababu zao.

Baadhi ya tabia za wanaume wa kaskazini mwa Papua New Guinea zinatokana na imani za kidini.

Moja ya mila hizo, zinaadhimishwa na watu wanaoishi katika eneo la Mto Sepik ambao wanaiga kuwa kama wanyama.

Image: BBC

Wanyama wanaowaheshimu sana ni pamoja na tai, nguruwe, nyoka na mamba.

Lakini mamba ndio wanajulikana kuwa na nguvu zaidi ya wanyama wote wanaoishi ndani au karibu na Mto Sepik.

Hivyo watu wa Sepik wakamfanya mamba kuwa mungu wao.

Moja ya sherehe za kuvutia zaidi duniani huhudhuriwa na wanaume wanaoishi karibu na mto huo wenye mtazamo wa kuvutia.

Huwa wanachora sehemu za miili yao kama vile mgongoni au mbele na kuunda miundo inayofanana na mamba, haswa wanapojificha kwenye maji ya mto kuwinda.

"Wavulana wanalelewa na shangazi zao ili kuendana na tamaduni. Muda wa kuasili tamaduni hiyo unaweza kuwa kuwa saa moja hadi mbili," alisema Aaron Malingi, mkuu wa wilaya ya Parambei.

Image: BBC

"Miaka mingi iliyopita, michoro hii katika miili ya wanaume hawa ilichorwa kwa mikuki mikali."

Ninapotazama miili ya wanaume hawa iliyochanika, nahisi uchungu wake.

"Baadhi ya wavulana maumivu yameisha tayari," Malingi alisema.

"Wanaume wakubwa hupakwa mafuta yaliyotolewa kwenye miti ili kuzuia kupata maambukizi."

Gavana wa eneo hilo alimweleza mwandishi wa habari kuwa, kwa mujibu wa imani yao, kitendo hicho kinalenga pia watoto wa kiume kumwaga damu za mama zao na kujipatia damu yao - jambo ambalo liliwashangaza wengi.

Baada ya wavulana hao kukeketwa, walikaa kwa miezi kadhaa ndani ya nyumba, wakijifunza kudhibiti maisha yao.

Image: BBC

Mafunzo haya hutolewa na wanaume waliopata mafunzo kama hayo tayari.

"Wanajifunza jinsi ya kuishi katika ujirani, na wanafundishwa jinsi ya kuvua samaki, kukata miti na jinsi ya kusaidia familia," Malingi alisema.

Mwandishi aliyeandaa taarifa hii aliuliza imekuwaje mamba kufikia hatua ya kuabudiwa na watu wa mkoa wa Sepik.

"Mamba wana nguvu ya mfano," Malingi alisema. "Tunawaogopa lakini tunapata nishati kutoka kwa uwezo wao."

Image: BBC

Alisema simulizi za kale ziliwaambia wanakijiji kwamba watu waliokuwa wakiishi hapo awali walikuwa wanyama kwenye mto ambao baadaye walikuja kuwa binadamu, na wakatoka nje.

Ndiyo maana walimchagua mamba na kumwabudu.

Lakini desturi ya kuabudu mamba imetoweka katika baadhi ya sehemu za jamii za mito ya Papua New Guinea.

Maeneo mengi yameachana na tamaduni hizo mnamo mwaka 1943, ingawa katika maeneo mengine kama eneo la Sepik bado utamaduni huo una nguvu.