Je, tabia ya kushindwa kudhibiti hisia zako za kufanya ngono ni ugonjwa gani?

Vitovu vya ubongo vinavyohusiana na hisia za kukupa furaha vinaweza kukosa nguvu kwa kukosekana kwa udhibiti wa ngono.

Image: BBC

Kwa miaka mingi tumesikia maneno kama "nymphomania" yaani "Uraibu wa kufanya ngono" au "kujamiiana", miongoni mwa maneno mengine ambayo huzungumzia kuhusu wale watu ambao wana matatizo ya kuwa na "hamu ya ngono iliyozidi au iliyopitiliza" au ukosefu wa udhibiti wa tabia zao za ngono.

Shirika la Afya Duniani (WHO) baada ya tafiti nyingi mwaka 2018 ilitambua "Ugonjwa wa kutoweza kudhibiti hisia za ngono".

Hali yao ikoje?

Vigezo vya uainishaji ugonjwa huu ni pamoja na watu ambao:

- Wamepoteza udhibiti wa tabia zao. - Wafanya jitihada za kuachana na tabia za ngono lakini hawawezi kuziacha. - Hawapati furaha yoyote kutokana na uzoefu huu. - Wana madhara makubwa katika maeneo mbalimbali ya maisha yao kwa zaidi ya miezi 6.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaelezea kwamba tatizo hili haliwezi kuelezwa na hukumu ya maadili, yaani, ukweli wa kwamba mtu haoni kama hii ni tabia nzuri au si nzuri kimaadili, hilo haliwezi kueleza kuwa kuna tatizo.

"Ngono imekuwa kama wasiwasi kwangu. Kila wakati nateseka na siwezi kuendelea tena na hali hii, kufanya ngono kumekuwa kimbilio langu ", mgonjwa mwenye umri wa miaka 45 alizungumza na BBC.

Ni kawaida kuchunguza jinsi wagonjwa wa tabia ya ngono wanavyokuwa (picha za ngono, ukahaba, kuwa na mazungumzo ya ngono kila wakati ama na mtu moja kwa moja au kwenye mitandao ya kijamii) ili kudhibiti ulimwengu wao wa mapenzi.

Wakati wagonjwa walio na matatizo haya hawajui jinsi ya kusimamia hisia zao, wao huenda kupata ngono ili kuwa na utulivu. Ingawa utafiti zaidi bado unahitajika, ugonjwa huu unaathiri karibu 10.3% ya wanaume na 7% ya wanawake katika jumla ya watu, kulingana na kitabu "compulible Sexual Behavior: A Comprehensive Look. A Guide for Professionals." 

Inaathiri vipi wale wanaoteseka na hali hiyo?

Watu walio na matatizo haya wanaweza kuathiriwa katika maeneo yafuatayo:

- Mtu binafsi: Njia ya kufikiri na kuelewa ngono ni potofu na kuna kupoteza heshima binafsi na kujiamini, hisia ya kutokuwa na uwezo, mabadiliko ya ustawi wa kiroho, adha binafsi, udhalilishaji au dharau, aibu, kujihisi kuwa na hatia na ukosefu wa maendeleo ya utambulisho binafsi.

- Kiuchumi: ukosefu wa ajira, matumizi mabaya ya fedha, ulaghai na udanganyifu.

- Uhusiano na wengine: Kutokuwa na hisia, kupoteza imani kwa wengine, matatizo katika mahusiano ya watu binafsi, uharibifu wa kihisia kwa wengine, kutengwa na jamii, kushindwa kuwa na upendo na wengine, kuvunjika kwa ndoa au mpenzi na kupoteza urafiki.

- Kitabibu: Magonjwa ya zinaa, mahusiano ya kimwili yasiyo na afya,  magonjwa ya akili, kutokuwa nah amu ya kufanya ngono na hali mbaya ya afya.

- Wengine: Matatizo ya kisheria (malalamiko, kukamatwa), tabia ya kutowajibika, mkengeuko wa malengo muhimu, kufukuzwa kutoka kwa mashirika, vyama, n.k. na kuzorota kwa taswira ya umma.

Tafiti maarufu zaidi za mfumo wa neva na jinsi ubongo unavyofanya kazi zimeonesha kwamba matatizo ya tabia ya ngono yanayoshurutisha yanaonyesha mabadiliko yanayofanana katika ubongo na yale yanayosababishwa na uraibu wa vitu vingine au tabia.

Vitovu vya ubongo vinavyohusiana na hisia za kukupa furaha vinaweza kukosa nguvu kwa kukosekana kwa udhibiti wa ngono.

Zaidi ya hayo, maeneo ya ubongo ambayo yanadhibiti kujidhibiti, kupanga, makini, na kujali kunaweza kubadilishwa kama inavyoonekana katika tafiti za hivi karibuni.

Namna ya kulitambua tatizo hilo

Baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza kutusaidia kushuku kwamba mtu anaugua tatizo hili ni:

- Kuwepo kwa msukumo, kutokuwa na uwezo wa kujidhibiti - Mabadiliko katika hisia kama vile kuwa na hasira, dalili kali na wasiwasi - Kuwepo kwa magonjwa ya zinaa

- Utegemezi wa teknolojia - Utendaji kazi wa kiwango cha chini au masomo na kukosa kwenda mara kwa mara

- Matumizi ya vilevi kama (pombe, tumbaku, bangi na vitu vingine) - Kushindwa kudhibiti kihisia zako - Upendeleo mkubwa wa kutafuta mambo mapya - Ugumu wa kujieleza kihisia. - Matumizi ya lugha ya mambo ya ngono kupita kiasi. - Matatizo ya utulivu kwa wanandoa, ukosefu wa uaminifu na kadhalika

- Hamu kidogo sana kingono na mpenzi wako - Kujihisi kuwa na hatia kweli kweli kuhusu vitendo vyako vya ngono.

- Kujihisi kuwa na hatia kweli kweli kuhusu vitendo vyako vya ngono.

Lakini kuna njia ya kupata suluhu ingawa ni ndefu na inahitaji uelewa, motisha, nguvu, msaada, uvumilivu, mapenzi, msaada na kujitolea, njia ya nje haipo.

Katika miaka ya hivi karibuni, matibabu tofauti yenye ufanisi yameonyeshwa kuwasaidia watu hawa, ikiwa ni pamoja na matibabu ya mtu binafsi (matibabu mbalimbali ingawa afya ya utambuzi yamejitokeza kuwa bora), matibabu yanayotolewa mukiwa kama kundi na wakati mwingine dawa.

Matibabu haya husaidia kudhibiti tabia na msukumo, pamoja na kujali afya ya uzazi na kuishi maisha huru. Pia kuna baadhi ya mafunzo ambayo yanaweza kusaidia kukuongoza kufanya maamuzi mema.