Kwa nini wakongwe wanahisi upweke enzi hii mambo mengi yakifanyika kidijitali?

Wengi wa wazee wanahisi wanafungiwa nje ya mambo muhimu kwa kukosa maarifa ya kutekeleza mambo kwa mfumo wa kisasa.

Muhtasari

• Mwingine alieleza kukosa chanjo ya Covid-19 si kwa sababu hakutaka bali kwa sababu mchakato wa kuitisha chanjo hiyo ulikuwa unafanyika kidijitali.

Mama mkongwe
Mama mkongwe

Katika kizazi hiki chenye uraibu wa mitandao ya kijamii na mambo ya kidijitali, watu wengi amabo umri wao umesonga wanahisi kupotea na kusahaulika na mambo, huku vijana wengi wakiofurahia usasa huu.

Kadiri huduma za kila siku zinavyozidi kuhamia kwenye mtandao, watu wazee na walio katika mazingira magumu hujihisi kufungiwa nje na hata kusahaulika kwani hawana weledi mkubwa wa kutumia mitandao ya kisasa kama vijana.

Wengi wa wazee hao wanaeleza kuwa wanahisi kupotea katika dunia ya usasa si kutokana na upweke au vifo vya wapenzi wao bali ni kutokana na kushindwa kukumbatia usasa ulioletwa na mifumo ya kidijitali.

Mwanamke mmoja mzee aliyekuwa akieleza jinsi usasa umewafungia nje mamilioni ya wazee alisema kadri mifumo ya mawasiliano ilivyobadilika pakubwa kidijitali, wengi siku hizi wanajuliana hali kupitia mitandao ya WhatsApp na mengine, simu yake iligoma kuita tena – kwani wengi siku hizi hawatumii mfumo wa kuandika jumbe fupi au kupiga simu moja kwa moja.

Hadithi ya mwanamke huyo kwa jina Doris, 87, kama ilivyosimuliwa na Makala ya Guardina, inaonyesha changamoto zinazowakabili mamilioni ya watu kote duniani kwani, wakati wa janga la Korona, huduma zaidi na zaidi zilihamishwa mtandaoni pekee.

"Kwake, mtandao ni kitu ambacho humzuia na kumfungia kufanya mambo ya ‘kawaida’. Jibu lake ni 'Kwa nini wanapaswa kufanya kila kitu kiwe ngumu sana wakati ninachotaka kufanya ni kuzungumza na mtu?' Ninaweza, na kufanya, kumsaidia kwa furaha kuuzunguka ulimwengu, lakini inanifanya nishangae jinsi watu walio katika mazingira magumu sawa, na hakuna wa kusaidia, anaweza kusimamia.’

Wazee wengi hawaelewi jinsi mifumo ya kisasa ya kupika vyakula inavyofanya kazi, haswa kutumia vyombo vya kielektroniki. Wengi wanategemea kutumia meko za kizamani au mitungi ya gesi ili kupika na kwao, mifumo hiyo mingine inachukua mud asana kabla chakula kiive.

Wengine walielezea jinsi walihisi kufungiwa nje haswa wakati wa kujisajili katika mfumo wa kupata chanjo, mchakato ambao ulikuwa unafanywa kupitia mtandao kwa simu za kidijitali.

“Tulijaribu kuweka nafasi ya chanjo, lakini hiyo lazima iwekwe mtandaoni na miadi ya karibu ilikuwa umbali wa maili 56," alielezea.

Si tu nchini Kenya bali nchini Uingereza pia watu wazee wanaishi kwa taharuki na hawana picha halisi jinsi maisha yao yatakavyokuwa kuanzia mwaka 2025 wakati simu za kizamani zitafungwa rasmi.

Wengine wanahisi kwamba ulimwengu kutokana na maoni ya watu wazee unatisha sana jinsi mambo yanakwenda haraka, mambo ambayo watu wadogo wanayachukulia kawaida sana bali kwa wazee ni fumbo la kutisha kwa sababu wao hawajui kuhusu teknolojia.