Atwoli aeleza alivyopata mali yake

Atwoli alisisitiza jinsi uamuzi wake wa kujiepusha na shughuli za kibiashara unamruhusu kudumisha uhusiano wa karibu na usio na doa na wafanyikazi.

Muhtasari
  • Masimulizi ya Atwoli yanatumika kama ukumbusho wa umuhimu wa kubaki mwaminifu kwa kanuni za mtu, haswa katika nyadhifa za uongozi.
Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli
Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli

Katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye kipindi cha JK na Jeff Koinange, Francis Atwoli, Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) nchini Kenya alifunguka kuhusu maoni yake kuhusu biashara, zabuni za serikali, na kujitolea kwa haki za wafanyakazi.

Atwoli, anayejulikana kwa haiba yake mahiri na utetezi thabiti wa haki za wafanyikazi, aliweka wazi kuwa lengo lake linasalia tu katika ustawi wa wafanyikazi.

Alijitenga na shughuli za kibiashara na zabuni za serikali akisema, "Sifanyi biashara. Siombi zabuni za serikali. Sina maslahi yoyote yanayokinzana na mwajiri yeyote".

Atwoli alisisitiza jinsi uamuzi wake wa kujiepusha na shughuli za kibiashara unamruhusu kudumisha uhusiano wa karibu na usio na doa na wafanyikazi.

"Mimi ni mtu anayelipwa 100% na hilo limenisongeza karibu na wafanyikazi", alisema, akielezea jinsi kujishughulisha na biashara, haswa na waajiri kunaweza kuathiri msimamo wake na kudhoofisha utetezi wake wa haki ya wafanyikazi.

Atwoli pia anashiriki maarifa kuhusu vishawishi vinavyokuja na uwezo na mali, akitahadharisha dhidi ya hatari zinazowakabili viongozi.

"Ikiwa leo, ningeenda kwa kampuni na  nikasema nataka kusambaza hii, wafanyakazi, siku iliyofuata wangejua kwamba mtu huyu anafanya biashara na anafanya biashara na nani? Ningeathirika", alifafanua.

Mazungumzo na Jeff aliangazia suala pana la viongozi wa Kenya kuyumbishwa na faida za kifedha, na kusababisha mabadiliko ya vipaumbele kutoka kwa majukumu yao ya kimsingi.

Masimulizi ya Atwoli yanatumika kama ukumbusho wa umuhimu wa kubaki mwaminifu kwa kanuni za mtu, haswa katika nyadhifa za uongozi.

Akiwa na taaluma iliyochukua zaidi ya miongo mitano, Atwoli ameweza kuishi maisha ya starehe na kukuza thamani yake na kuwa miongoni mwaWakenya wenye ushawishi mkubwa zaidi.