(Picha) Maduka yafungwa jijini Nairobi wakenya wanaposibiri matokeo ya urais

Hali ya wasiwasi imetanda kote nchini huku maduka mengi tayari yakiwa yamefungwa katika jiji kuu la Nairobi.

Muhtasari

• Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema matokeo hayo yangetangazwa mwendo wa saa tisa alasiri.

•Hali ya wasiwasi imetanda kote nchini huku maduka mengi tayari yakiwa yamefungwa katika  jiji kuu la Nairobi.

Maduka kando ya mitaa ya Tom Mboga yamefungwa watu wameondoka.
Maduka kando ya mitaa ya Tom Mboga yamefungwa watu wameondoka.
Image: FREDRICK OMONDI

Wakenya kote nchini wamesubiri kwa hamu na ghamu matangazo ya matokeo ya urais kutangazwa na tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC).

Kupitia barua ya mwaliko kwa vyombo vya habari Jumatano asubuhi , Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema matokeo hayo yangetangazwa mwendo wa saa tisa alasiri.

Hata hicho kumekuwa na kuchelewa kwa matangazo ya matokeo hayo kufuatia sababu zisizothibitishwa.

Huku Wakenya wakisubiri kujua hatima ya uchaguzi uliofanyika Jumanne wiki jana, hali ya wasiwasi imetanda kote nchini huku maduka mengi tayari yakiwa yamefungwa katika  jiji kuu la Nairobi.

Tazama hali ilivyo Nairobi hapa:-

Maduka kando ya mitaa ya Tom Mboga yamefungwa watu wameondoka
Maduka kando ya mitaa ya Tom Mboga yamefungwa watu wameondoka
Image: FREDRICK OMONDI
Mtaa wa Taifa ni tupu watu wameondoka.
Mtaa wa Taifa ni tupu watu wameondoka.
Image: FREDRICK OMONDI