Uingereza yajutia dhulma zilizofanywa dhidi ya Wakenya enzi ya ukoloni

Ripoti iliyotolewa kwa umma siku ya Jumatatu iliangazia jinsi watu katika eneo la magharibi mwa Kenya- ambayo sasa ni jimbo la Kericho walivyodhulumiwa.

Muhtasari

•Serikali ya Uingereza imesisitiza msimamo wake "dhidi ya adhabu ya kikatili, isiyo ya kibinadamu, na ya kudhalilisha" kujibu ripoti ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa unaoangazia jinsi Wakenya walivyodhulumiwa na mamlaka ya kikoloni ya Uingereza mwishoni mwa Karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.

Image: BBC

Serikali ya Uingereza imesisitiza msimamo wake "dhidi ya adhabu ya kikatili, isiyo ya kibinadamu, na ya kudhalilisha" kujibu ripoti ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa unaoangazia jinsi Wakenya walivyodhulumiwa na mamlaka ya kikoloni ya Uingereza mwishoni mwa Karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.

Ripoti iliyotolewa kwa umma siku ya Jumatatu iliangazia jinsi watu katika eneo la magharibi mwa Kenya- ambayo sasa ni jimbo la Kericho walivyodhulumiwa.

Waandishi wa ripoti hiyo walikuwa wameikabidhi mwishoni mwa Mei na kupatia mamlaka ya Uingereza siku 60 kujibu.

Hakuna jibu lililotolewa kwa na wachunguzi wa UN - wanaojulikana kama waandishi wa habari maalum - wameelezea kusikitishwa kwamba hakuna msamaha uliotolewa kwa kile kilichotokea wala hoja ya fidia.

Katika jibu lililotumwa kwa BBC, msemaji wa serikali alisema:

“Taarifa ya Serikali ya Uingereza iliyotolewa mnamo 2013, kuwatambua wahanga wa mateso na unyanyasaji wakati wa kipindi cha dharura, ilikuwa sehemu ya kusuluhishwa na Serikali ya Uingereza ya madai yaliyotolewa na raia wa Kenya.

“Tunasikitika kwamba unyanyasaji huu ulifanyika, na kwamba uliathiri maendeleo ya Kenya kuelekea uhuru."