Wafanyibiashara wawili waliopatikana na lita 740 za chang'aa Kisumu watozwa faini ya 640,000

Beatrice Awino na Jackson Wanga watalazimika kuhudumu kifungo cha miezi sita iwapo watashindwa kulipa faini hizo.

Muhtasari

•Kando na kuendeleza biashara haramu, wawili hao walipatikana na hatia ya kumiliki mifuko iliyopigwa marufuku ya plastiki ambayo walikuwa wanatumia kuuza kileo cha chang'aa.

•Awino na Wanga walipatikana na lita 740 za chang'aa iliyokuwa imewekwa kwa vibuyu 36.

Beatrice Awino na Jackson Wanga ambao walipatikana wakiuza changaa
Beatrice Awino na Jackson Wanga ambao walipatikana wakiuza changaa
Image: MAURICE ALAL

Habari na Maurice Alal

Mahakama ya Kisumu imetoza watu wawili faini ya shilingi 320,000 kila mmoja baada ya kupatikana na ahatia ya kuuza pombe haramu.

Beatrice Awino na Jackson Wanga watalazimika kuhudumu kifungo cha miezi sita iwapo watashindwa kulipa faini hizo.

Wawili hao walikamatwa mnamo Jumapili asubuhi walipokuwa wanauza chang'aa katika maeneo ya Obunga, Kisumu ya kati.

Awino na Wanga walipatikana na lita 740 za chang'aa iliyokuwa imewekwa kwa vibuyu 36.

Kando na kuendeleza biashara haramu, wawili hao walipatikana na hatia ya kumiliki mifuko iliyopigwa marufuku ya plastiki ambayo walikuwa wanatumia kuuza kileo cha chang'aa.

Mahakama ilitoa agizo kuwa pombe haramu iliyopatikana iharibiwe kulingana na sheria.