Kenya imepokea dozi zingine 55,000 za chanjo ya astrazeneca

Muhtasari

Kenya imepokea dozi zingine 55,000 za chanjo ya astrazeneca

Image: Twitter/MoH

Kenya imepokea dozi zingine  55,000 za chanjo ya astrazeneca kutoka  kwa serikli ya Latvia.

Chanjo hizo ziliwasili nchini Jumamosi asubuhi, kuleta idadi ya dozi ya chanjo ya Covid-19 iliyopatikana nchini hadi 4,266,500.

Chanjo zilipokelewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ununuzi wa Chanjo  John Kibuchi na Balozi wa Kisheria kwa EU nchini Kenya Katrin Hagemann katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

"Tunataka kushukuru msaada ambao tumepokea kutoka kwa watu wa Latvia," Kibuchi alisema.

Hagemann kwa upande wake alisema hii ilikuwa shehena maalum ikizingatiwa kuwa Latva hana uwepo katika bara la Afrika.

"Tulipeleka ombi kwamba Kenya inahitaji chanjo zaidi na walijibu na kwa msaada wa Mfumo wa Ulinzi wa Raia wa Muungano tuliweza kusaidia usafirishaji kwenda Kenya," alisema.

Chanjo hizo zilikuja masaa kadhaa baada ya Kenya kupokea dozi 141,000 za chanjo ya Johnson and Johnson.

Katibu mwandamizi wa wizara ya afya Mercy Mwangangi ambaye alipokea shehena hiyo kwa niaba ya CS Sen Seneta Mutahi Kagwe aliwauliza Wakenya kupata chanjo  akisema kuwa serikali imeongeza upatikanaji wa chanjo .

"Napenda pia kuwaomba wale ambao tayari wamepokea kipimo chao cha kwanza cha AstraZeneca kuhakikisha kuwa wanaendelea na kupata kipimo chao cha pili. Sasa tuna vituo vya kutosha ndani ya nchi ili kusiwe na kusita wakati wa kuja kupata kipimo chako cha pili cha AstraZeneca, "Mwangangi alisema.