CBK yaagiza mamilioni ya wakenya waondolewe kwenye orodha ya CRB

Muhtasari
  • CBK yaagiza mamilioni ya wakenya waondolewe kwenye orodha ya CRB
cbk governor
cbk governor

Benki Kuu ya Kenya (CBK) mnamo Jumatatu, Novemba 8, ilitangaza kusimamisha uorodheshaji hasi wa mikopo kwa waliokopa Ksh 5milioni na chini kwa muda wa miezi 12.

Katika taarifa ya CBK ilisema kuwa agizo hilo lilianza kutekelezwa kuanzia Oktoba 1 na litakamilika Septemba 30, 2022.

Agizo hilo lilitolewa kuambatana na tangazo la Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe za siku ya Mashujaa.

Uhuru alibainisha kuwa hatua hiyo ni mojawapo ya hatua anazochukua kuinua uchumi wa Kenya kutokana na athari za janga la kimataifa.

"Wakala hutangaza kusimamishwa kwa muda wa miezi kumi na mbili ya kuorodhesha habari mbaya za mikopo kwa wakopaji walio na mikopo iliyo chini ya Ksh5 milioni ambao mikopo yao ilikuwa ikifanya kazi hapo awali lakini imekuwa haifanyi kazi kuanzia Oktoba 1 2020

Zaidi ya hayo, CRB hazitajumuisha katika ripoti yoyote ya mikopo, taarifa yoyote mbaya ya mikopo ya mteja chini ya Ksh5 milioni iliyowasilishwa kwa CRB kuanzia Oktoba 1, 2020, hadi Septemba. 30, 2021," Ilisoma taarifa ya CBK.

Zaidi ya Wakenya milioni 14 wameorodheshwa kwenye Taasisi za Marejeleo ya Mikopo (CRBs) - na kuathiri pakubwa upatikanaji wa mikopo wakati mamilioni ya watu wakipoteza kazi.