Watoro wa Kamiti wakiri kutoroka gerezani, wakanusha kutenda kitendo cha kigaidi

Muhtasari
  • Watoro wa Kamiti wakiri kutoroka gerezani, wakanusha kutenda kitendo cha kigaidi
Musharraf Abdalla, Joseph Juma na Mohammed Abdi wakamatwa wakielekea Somalia
Musharraf Abdalla, Joseph Juma na Mohammed Abdi wakamatwa wakielekea Somalia
Image: HISANI

Wafungwa watatu waliotoroka jela ya Kamiti Jumatatu walikiri kutoroka gerezani, lakini wakakana kutekeleza shughuli zozote za kigaidi.

Wakifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Diana Mochache katika Mahakama ya Sheria ya Kahawa, watatu hao; Musharraf Abdalla Akhulunga alia Zarkarawi, Mohammed Ali Abikar na Joseph Juma Odhiambo almaarufu Yusuf ambao pia walikuwa pamoja na mshtakiwa wa nne walikiri shitaka la kutoroka kifungo halali cha washtakiwa watatu.

Hata hivyo, walikanusha shtaka jingine ambapo walituhumiwa kufanya kitendo cha kigaidi kwa kutoroka gerezani, jambo ambalo lilikuwa tishio kwa usalama wa taifa.

Mshtakiwa wa nne, Abdulmajid Yassin alishtakiwa kwa kusaidia kutoroka kwa wafungwa wengine watatu kutoka Kamiti Maximum.

Alikanusha shtaka.

Watatu hao wanadaiwa kutoroka katika gereza kuu la Kamiti mnamo Novemba 14, 2021.