Wakenya washiriki kampeni kushinikiza serikali kupunguza bei ya vyakula

Muhtasari

•Wakenya wengi wamelalamika kuwa wanasongwa na gharama kubwa ya maisha kufuatia kupanda kwa bidhaa za kimsingi kama vile mafuta, mchele, unga wa ugali, sukari

Vyakula mbalimbali sokoni
Vyakula mbalimbali sokoni
Image: MERCY MUMO

Wakenya kupitia mitandao ya kijamii wameshiriki kampeni  ya kushinikiza serikali iweze kupunguza bei za bidhaa ya vyakula humu nchini.

Kampeni hiyo inaendelezwa kwenye mitandao yote ya kijamii,ikiwemo Facebook, Instagram na Twitter chini ya alama reli ‘#lowerfoodprices’

Wakenya wengi wamelalamika kuwa wanasongwa na gharama kubwa ya maisha kufuatia kupanda kwa bidhaa za kimsingi kama vile mafuta, mchele, unga wa ugali, sukari nk.

Wanaeleza kuwa kuweka mlo mezani limekuwa jambo ngumu kwa Mkenya wa kawaida huku wakifichua kuwa familia nyingi humu nchini zinalala njaa kutokana na kushindwa kununua chakula kutokana na bei ilivyo kwa sasa.

Wengi wa watu mashuhuri wameonekana kuungana na wakenya kushinikiza serikali kupunguza bidhaa ya hizo muhimu.

Baadhi ya vyakula ambazo  zimepanda ni ikiwemo na  mafuta ya kupika ambayo lita  moja inagharimu 320, Sukari kilo mbili 280.

Baadhi ya maoni ya Wakenya  ni kama;

@Mike Sonko-wakati gharama ya uzalishaji ni kubwa tarajia bei  kuwa juu. Siku hizi hatanikipea mtu elfu moja najua tu labda anunue 2kg ya sukari na 2kilo mbili za mafuti ya kupikia.

@Ustad, LordAbraham Mutai - Wale wanaopiga kelele za #LowerFoodPrices walipigia kura mara tatu UHURUTO kumrudisha Raila Odinga nyumbani. Wanapanga kumpigia kura William Ruto ili kumrudisha Uhuru Kenyatta nyumbani.

@KuriaKimaniMP- Kupunguza gharama za uzalishaji kwa kupunguza gharama ya mbolea itakuwa hatua nzuri ya kupunguza gharama ya chakula.Nilitafuta taarifa.