Sikumaanisha Karua, Kindiki aomba msamaha kwa ajili ya orodha ya wageni wa UDA

Muhtasari
  • Msamaha wake unajiri baada ya kiongozi huyo wa Narc Kenya kukanusha kuwa atahudhuria hafla ya Muungano wa UDA
EYYPE_hWsAELaEP
EYYPE_hWsAELaEP

Seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki ameomba msamaha kuhusu matamshi kwamba kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua atahudhuria Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa UDA mnamo Jumanne.

Katika taarifa, Kindiki alisema ni kuteleza na kwamba alimaanisha kusema kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.

"Kwa kutojua, kuteleza kwa unyoofu, nilimrejelea "Kiongozi wa Ford Kenya Martha Karua" anayetarajiwa kuhudhuria UDA NDC kesho. Nilimaanisha Ford Kenya Moses Wetangula," alisema.

"Samahani kwa Wetangula na Karua, na vyama vyao vya kisiasa kwa mchanganyiko huo."

Msamaha wake unajiri baada ya kiongozi huyo wa Narc Kenya kukanusha kuwa atahudhuria hafla ya Muungano wa UDA.

Kupitia kwenye ukurasa wa twittert, Karua ambaye alikuwa ameombwa kuthibitisha kama atahudhuria UDA NDC Jumanne alisema "Si Kweli".

"Tunawatarajia wageni wengine akiwemo Martha Karua lakini hatutasema majina yao kwa sasa," Kindiki alisema alipokuwa akihutubia mkutano na wanahabari kuhusu NDC Jumatatu.