Maisha London kwa wafanyakazi wa KRA wanaonyonyesha, kutengewa chumba, kupunguziwa saa za kazi

Muhtasari

• Mamlaka yacukusanyaji kodi KRA imetangaza kuzindua chumba cha kunyonyeshea watoto katika ofisi zake.

• KRA pia imetangaza manufaa mengine ambayo kina mama wanaonyonyesha watapokea wakiwa kazini.

Uzinduzi wa chumba cha kunyonyeshea watoto Kisumu
Uzinduzi wa chumba cha kunyonyeshea watoto Kisumu
Image: KRA//Facebook

Aprili mosi, mamlaka ya ukusanyaji kodi nchini KRA ilizindua chumba cha kina mama kunyonyesha watoto wao nyakati za kazi pindi wanaporejea kutoka likizo ya kujifungua.

“Tulizindua chumba cha kunyonyesha katika makao makuu ya Mkoa wetu wa Kisumu kupitia Mkuu wetu wa Mkoa wa Magharibi mbele ya Mwakilishi wetu wa HR na wafanyikazi wa Kisumu,” KRA walifurahia kuripoti kupitia Facebook yao.

Kulingana na KRA, chumba hicho kitakuwa kimeundwa kwa njia ya kipekee na kitakuwa na umaaluma unaowapa kina mama amani ya nafsi wanaponyonyesha watoto wao.

Kulingana na takwa la katibu la mwaka 2017 kuhusu afya, kilasehemu ya kazi ilitakiwa kuwa na chumba kilichotengwa kwa ajili ya kina mama kunyonyesha watoto na chumba hicho kinapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo.

  • Ulinzi dhidi ya kuonekana na kuwa huru kutokana na kuingiliwa na wafanyakazi wenza
  • Kuwa safi, tulivu, faragha, na chenye joto zuri
  • Kisiwe maeneo ya bafuni au chooni
  • Kuwa na mlango unaofungwa
  • Kuwa na beseni la kuogea
  • Kuwa na friji kwa ajili ya kuhifadhia maziwa yaliyokamuliwa
  • Kuwa na mpangilio wa sehemu ya umeme na taa
  • Kuwa na kiti, meza, na nafasi safi ya kuhifadhia vifaa miongoni mwa vigezo vingine.

Kando na kuanzisha kutenga vyumba hivyo, mamlaka ya KRA pia ilisema inawapa wanawake wanaoenda kujifungua likizo ya miezi mitatu ambayo wanawalipa na pindi wanaporudi kazini, kina mama hao wanapunguziwa saa za kufanya kazi, ili kutoa nafasi nzuri kwa kujenga ukaribu wa mama-mtoto, ambayo ilitajwa na shirika la UNICEF kuwa na manufaa makubwa katika makuzi ya mtoto.