Tuna muda wa kutosha, usajili wa laini za simu unaweza subiri-Ruto

Muhtasari
  • Ruto alisema kwa sasa nchi inakabiliwa na mizozo kadhaa yenye thamani zaidi kuliko zoezi la usajili wa laini
DP RUTO
Image: DOUGLAS OKIDDY

Naibu Rais William Ruto amekosoa usajili unaoendelea wa SIM kadi ambao umeshuhudia mamia ya Wakenya wakipanga foleni katika wafanyabiashara wa laini za simu.

Akizungumza Jumanne wakati wa kutia saini mikataba ya muungano na vyama vinane katika Ngonga Racecourse, Nairobi, DP alisema kuwa hakuna haja ya kuharakisha zoezi hilo.

Ruto alisema kwa sasa nchi inakabiliwa na mizozo kadhaa yenye thamani zaidi kuliko zoezi la usajili wa laini.

"Nataka kuwauliza watu wetu katika CA, tafadhali, sio lazima kwao kupanga foleni ya sim card ili wasajiliwe. Tuna muda wa kutosha, ni uchawi gani huu kuhusu Ijumaa?" Ruto aliuliza.

Aliongeza kuwa zoezi hilo linaweza kusubiri na kwamba tarehe ya mwisho ya Aprili 15 inaweza kusukumwa hadi Desemba.

"Isipokuwa huna lolote. Ikiwa CA ni wakala wa nguvu za giza, tunataka kuwaambia, watashindwa, na watashindwa vibaya."