Fedha za Kazi Mtaani hazitumiki kwa Kampeni-Kibicho

Muhtasari
  • Serikali inapanga kutumia Sh5 bilioni chini ya mpango unaoendelea unaohusisha vijana
Katibu wa kudumu wa mambo ya ndani Karanja Kibicho katika mahojiano ya Radio Jambo siku ya Jumatano, Februari 23, 2021.
Katibu wa kudumu wa mambo ya ndani Karanja Kibicho katika mahojiano ya Radio Jambo siku ya Jumatano, Februari 23, 2021.
Image: MINISTRY OF INTERIOR

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Karanja Kibicho amekanusha madai kwamba serikali inawalipa malipo duni vijana walioajiriwa chini ya Kazi Kwa Vijana na kuelekeza fedha kwa ajili ya kampeni.

Alisema kinyume na madai ya baadhi ya wanasiasa, Sh450 zinazolipwa kila siku kwa vijana wanaojishughulisha na Mpango wa Kitaifa wa Usafi wa Mazingira ni kiasi ambacho kimetengewa bajeti na ambacho kimekuwa kikilipwa kwa walengwa tangu kuzinduliwa kwake 2020.

Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua na wabunge wengine ambao wamedai kuwa Bunge la Kitaifa lilikuwa limetenga angalau Sh1,000 za posho ya kila siku kwa kila kijana anayehusika na mpango huo kote nchini kuwasilisha ushahidi unaounga mkono.

“Ningetaka watoe ripoti ya Hansard kuthibitisha hoja yao kwamba kweli, Wabunge walitunga sheria ya kiasi wanachodai. Hili linafaa kuwa rahisi kuthibitisha kwani Bunge ni Nyumba ya kumbukumbu,” PS alisema.

PS aliyekuwa akizungumza kwenye kituo cha Kameme FM alisema vijana 530,608 ambao wamejishughulisha na kipindi hicho wamekuwa wakipokea kiasi hicho tangu Kazi Mtaani ilipozinduliwa.

Serikali inapanga kutumia Sh5 bilioni chini ya mpango unaoendelea unaohusisha vijana katika shughuli zinazohitaji nguvu kazi kama vile kufanya usafi mijini na ujenzi wa miradi ya miundombinu inayofadhiliwa na umma.

Bajeti ya hivi punde zaidi itasukuma matumizi ya chini ya mpango huo hadi Sh21 bilioni.

Waziri huyo aliendelea kukanusha madai kuwa mpango huo ulikuwa unatumiwa kuwarubuni wapiga kura kumuunga mkono mgombeaji urais wa Azimio Raila Odinga, akisema kuwa ugavi wake uligawanywa na kuwaajiri walengwa kulifanyika mashinani kote nchini.

"Inawezekanaje kujua ni vijana gani wanashirikiana na mwanasiasa gani kama sharti la kupata kazi hizi? Uajiri unafanywa katika ngazi ya chini kabisa ya utawala na machifu na wasaidizi wao ambao wana nafasi nzuri ya kujua wanaofaa zaidi kwa nafasi zilizopo,”