Mwanafunzi wa kidato cha 3 awachoma kisu dada wawili mara 28

Jane Kibe mwenye umri wa miaka 48 na dadake Peris Wanjiru mwenye umri wa miaka 35 wanauguza majeraha mabaya

Muhtasari
  • Alifanya kitendo hicho Jumatatu mchana alipoingia ndani ya nyumba hiyo na kujifungia ndani na kuwashambulia wawili hao
Image: BEN NDONGA

Mvulana wa kidato cha tatu amewashangaza wakazi wa Laikipia baada ya kuwadunga kisu dada wawili katika kaunti hiyo na kuwaacha wakidhani wamekufa.

Jane Kibe mwenye umri wa miaka 48 na dadake Peris Wanjiru mwenye umri wa miaka 35 wanauguza majeraha mabaya ya kudungwa kisu mara 19 na 9 mtawalia.

Inadaiwa kuwa yeye ni mtoto wa mmoja wa wagombea ubunge huko Gilgil.

Alifanya kitendo hicho Jumatatu mchana alipoingia ndani ya nyumba hiyo na kujifungia ndani na kuwashambulia wawili hao.

Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Peter Mwanzo, mshukiwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Gilgil na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya jaribio la mauaji.