Malkia Elizabeth II: Maisha katika picha

Wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu, Elizabeth na dada yake Margaret walihamishwa hadi Windsor

Muhtasari

• Katika miaka yake ya mapema, hakuna mtu ambaye angeweza kutabiri kwamba kiti cha ufalme kingekuwa hatima yake.

Image: PA MEDIA

Malkia Elizabeth II aliishi maisha yake akiangaziwa pakubwa . Tunatazama nyuma katika enzi yake, kutoka akiwa mtoto hadi mrithi mtawala wa kifalme aliyetawala muda mrefu zaidi wa Uingereza.

Image: PA MEDIA

Elizabeth Alexandra Mary Windsor alizaliwa tarehe 21 Aprili 1926, katika nyumba karibu na Berkeley Square huko London. Alikuwa mtoto wa kwanza wa Albert, Duke wa York - mtoto wa pili wa George V - na mkewe, Lady Elizabeth Bowes-Lyon wa zamani.

Image: GETTY IMAGES

Katika miaka yake ya mapema, hakuna mtu ambaye angeweza kutabiri kwamba kiti cha ufalme kingekuwa hatima yake.

Image: GETTY IMAGES

Hata hivyo, ilisemekana kuwa alionyesha hisia ya ajabu ya uwajibikaji tangu umri mdogo sana.

Image: GETTY IMAGES

Elizabeth na dada yake, Margaret Rose, aliyezaliwa mwaka wa 1930, walisoma nyumbani.

Image: GETTY IMAGES

Kufuatia kusalimisha kiti cha ufalme na Mfalme Edward VIII mnamo 1936, babake Elizabeth alikua George VI na akawa mrithi.

Image: TOPICAL PRESS AGENCY / GETTY IMAGES

Wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu, Elizabeth na dada yake Margaret walihamishwa hadi Windsor. Picha hii inawaonyesha wakitangaza kwa taifa katika kipindi cha Children's Hour kwenye idhaa ya BBC.

Image: AFP

Binti wa kifalme alijiunga kwa muda mfupi na Huduma ya Auxiliary Territorial Service (ATS) mwishoni mwa vita alipojifunza kuendesha gari na kuyafanyia ukarabati.