Mvuvi aliyesaidia kuokoa abiria 24 wa ndege iliyozama atuzwa kwa Sh 50,000

Pia aliahidiwa kuajiriwa kwenye kikosi cha uokoaji

Muhtasari

•Mvuvi huyo alituzwa na kima cha shilingi Milioni moja za Tanzania (takriban Ksh 50,000) kutokana na ushupavu ambao alionyesha.

Jackson Majaliwa atuzwa milioni moja kwa kuwaokoa watu 24
Jackson Majaliwa atuzwa milioni moja kwa kuwaokoa watu 24
Image: Facebook

Kijana mmoja Mtanzania aliingia kwenye vitabu vya mashujaa nchini humo baada ya kuwaokoa  watu 24 kwenye mkasa wa ndege ambayo ilipata hitirafu na kuanguka ziwa la Victoria wikendi iliyopita.

Kijana huyo anayefamika kama Jackson Majaliwa alituzwa na kima cha shilingi Milioni moja za Tanzania (takriban Ksh 50,000) kutokana na ushupavu ambao alionyesha.

Pesa hizo ambazo alikabithiwa na na mkuu wa mkoa Albert Chalamila ikiwa kama njia ya kumpa pongezi na shukrani sufufu kufuatia kitendo chake cha ushujaa huku waziri huyo akimuahidi ajira kwenye kikosi la uokozi.

''Rais Samia Suluhu Hassan, ameagiza kijana aliyejitosa majini kuwaokoa abiria, Majaliwa Jackson, ameagiza akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ili apatiwe nafasi katika Jeshi la Uokoaji kwa ajili ya mafunzo.''  Alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Inadaiwa kijana huyo ambaye ni mvuvi, alikuwa kwenye pilka pilka zake za uvuvi hadi wakati alipoona ndege hiyo ya aina ya Precision Air ikitumbukia kwenye ziwa na bila kusitasita akaogolea na kuwatengezea njia ya kutokea abiria waliokuwa wamekwama.

Waziri huyu alimkabithi pesa hizo wakati taifa lilikuwa linawaanga miili ya watu 24 walioipiga dunia teke kwenye ajali hiyo ya kuhuzunisha.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera amesema, kama si kitendo kilichofanywa na kijana huyo, idadi ya watu waliofariki dunia huenda ingekuwa kubwa zaidi.