Sonko ajitolea kuendesha ndege za KQ kufuatia mgomo wa marubani ulioathiri usafiri

Sonko alisema ana ujuzi wa kuendesha ndege yoyote ile na kudai anaweza kuwa rubani bora.

Muhtasari

• Sonko amedokeza azma yake ya kujitosa kwenye kazi wazo  urubani katika shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) iliyotatizika wiki iliyopita kutokana na mgomo wa marubani.

• Aliongeza na kusema anaweza kutengeneza kipato kutokana na  ujuzi wake wa kuendesha ndege.

Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amedokeza azma yake ya kujitosa kwenye kazi wazo  urubani katika shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) iliyotatizika wiki iliyopita kutokana na mgomo wa marubani.

Siku ya Jumapili, Sonko kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema ana ujuzi wa kuendesha ndege yoyote ile na kudai anaweza kuwa rubani bora wa kutoa huduma ya kuendesha ndege za KQ kabla ya mgogoro baina ya marubani na wasimamizi wa shirika hilo la usafiri wa ndege kutatuliwa.

Mfanyibiashara huyo alichapisha video iliyomuonyesha akiendesha ndege na chini yake kusema ''Nina uzoefu mzuri sana. Ninaweza kuendesha ndege yoyote hadi mahali popote pale ulimwenguni''

Aliongeza na kusema anaweza kutengeneza kipato kutokana na  ujuzi wake wa kuendesha ndege. Aidha alidai mchango wake utawafaidi wasafiri na watalii ambao wanalalamika kwamba ziara zao zitatatizika iwapo mgomo huo utaendelea kwa muda mrefu bila suluhu kupatikana.

Mgomo unaoendelea ulitokea baada ya matakwa ya marubani kudaiwa kutotimizwa na Afisa mtendaji wa shirika hilo Allan Kilavuka ambaye alisema hatua hiyo ya marubaini ni kinyume na sheria na imepitwa na wakati.

Hali tete inayojitokeza ni iwapo mgomo huu utandelea kwa muda mrefu kwani itasababisha shughuli za ndani na za nje ya nchi kuzorota hivyo kudorora kwa uchumi.

Mgomo huu unalioaza mnamo Novemba 5ambao unakisiwa kuaadhiri sekta ya utalii ambayo hupokea zaidi ya maelefu ya watalii wanaokuja kujiburudisha haswa msimu tunaelekea wa krisimasi.