Rais Ruto: Kulikuwa na njama ya kumteka nyara na kumuuwa Wafula Chebukati

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na makamishna Abdi Guliye na Boya Molu walistaafu Januari 17 baada ya kipindi cha miaka 6 kukamilika kikatiba.

Muhtasari

• Ruto katika hotuba yake watatu hao wakiondoka ofisini, alisema kuwa vitisho vilikuwa vingi dhidi yao lakini walisimama tisti.

• Alisema kuwa waliahidiwa zawadi nono lakini hilo halikuwashawishi kubatilisha uchaguzi wa wananchi.

Chebukati alitunukiwa heshima ya kiraia ya EGH na rais William Ruto.
Chebukati alitunukiwa heshima ya kiraia ya EGH na rais William Ruto.
Image: Twitter

Jumanne January 17, makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC walikuwa wanamaliza muda wao wa miaka 6 katika tume hiyo kulingana na agizo la katiba.

Makamishna hao watatu waliosalia na ambao walikuwa wanastaafu rasmi ni pamoja na mwenyekiti Wafula Chebukati, Abdi Guliye na Boya Moyu ambao walisalia na kuwa na msimamo knzani na ule wa wale wane ambao walijiternga na matokeo na baadae kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

Hafla ya kustaafu rasmi kwa watatu hao kutoka IEBC iliandaliwa jijini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais William Ruto ambaye awali amenukuliwa mara kadhaa akimtaja Chebukati kama shujaa aliyesimamamia ukweli katika uchaguzi wa Agosti mwaka jana.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, rais Ruto alisisitiza kuwa wana ufahamu kuwa kulikuwepo na njama na kumteka nyara mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na kumuua baada ya kukataa kukubaliana na kile ambacho Ruti alisema ni kurubuni kwa matokeo ghushi ya kumtangaza mpinzani wake Raila Odinga kama rais.

“Pia tuna habari kuwa kulikuwepo na jaribio la moja kwa moja la kumteka nyara Wafula Chebukati na kumuua ili tume ya IEBC ilemazwe au kamishna mbadala achukue hatamu na kubatilisha kile ambacho wananchi walikuwa wameamua. Ulikuwa ni wakati mgumu, vitisho vilikuwa vingi, ahadi za kumezewa mate nyingi na shinikizo lilikuwa juu,” Rais Ruto alisema.

Alizidi kusema kuwa Chebukati na wenzake watatu hawakukubali kurubuniwa na vyote hivyo na walisimama katika njia kuu na kukana majaribio hayo yote ambayo yalinuia kubatilisha uamuzi wa wananchi debeni.

Mwaka jana katika sherehe za Jamhuri, Rais Ruto alimtunuku Chebukati na wengine wengi tuzo ya heshima ya kirais ya OGW kama mmoja wa mashujaa katika mwaka huo.

Aidha, jarida la The Star lilimtaja Chebukati kama mtu aliyefana zaidi nchini kwa mwaka huo, katika chapisho ambalo huchapishwa kila mwisho wa mwaka kufuatia kura ambazo wananchi hupiga kumchagua mtu katika kitengo cha ‘Star Person of the Year’.