Duale aifariji Uturuki baada ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000

Majengo mengi yameporomoka na timu za uokoaji zimetumwa kutafuta manusura chini ya lundo kubwa la vifusi.

Muhtasari
  • Rais Recep Erdogan alisema kuwa hawezi kutabiri kama idadi ya vifo itaongezeka huku juhudi za uokoaji zikiendelea
ADEN DUALE
Image: EZEKIEL AMINGA

Waziri wa Ulinzi Aden Duale ametuma ujumbe wa rambirambi kwa Uturuki kufuatia tetemeko kubwa la ardhi Jumatatu asubuhi.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha Richter lilitokea kusini-mashariki mwa Uturuki, karibu na mpaka wa Syria, na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

"Ninaungana na ulimwengu wote kuelezea wasiwasi wangu na kutoa rambirambi zangu kwa watu na familia zilizoathiriwa, na serikali ya Uturuki," Duale alisema.

Rais Recep Erdogan alisema kuwa hawezi kutabiri kama idadi ya vifo itaongezeka huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Makadirio ya hivi punde tuliyo nayo kwa Syria, ambayo yanatoka katika Kituo cha Kuchunguza Haki za Kibinadamu cha Syria chenye makao yake nchini Uingereza, ni 320.

Nchini Syria, zaidi ya watu 50 waliuawa, vyombo vya habari vya serikali viliripoti. Kuna hofu kwamba idadi ya vifo itaongezeka sana katika saa zijazo.

Majengo mengi yameporomoka na timu za uokoaji zimetumwa kutafuta manusura chini ya lundo kubwa la vifusi.