Huzuni! Familia yawapoteza watoto 3 katika ajali ya barabarani Kiambu

"Walikuwa wameenda kumchukua dada yao kisha wanarudi. Nisingejua wamejikutaje hapa kwenye ajali hii," alisema.

Muhtasari
  • Mama huyo alipokuwa akisimulia mkasa huo mchungu, alieleza kwamba wanne hao walimwambia walikuwa sawa mara ya mwisho alipozungumza nao.
Ajali
Ajali
Image: HISANI

Familia moja iliyoko Kiambu iko katika majonzi baada ya watoto wao wanne kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani.

Mama wa watoto hao alieleza kuwa watatu kati yao walifariki dunia wakiwa ICU. Mmoja wao alinusurika kwenye ajali hiyo.

"Walikuwa wameenda kumchukua dada yao kisha wanarudi. Nisingejua wamejikutaje hapa kwenye ajali hii," alisema.

Gazetti la The Star halikuweza kufichua jinsi ajali hiyo ilivyotokea wakati wa kuchapisha habari hii.

Hata hivyo, eneo la tukio lilikuwa na lori lililokuwa na skrini iliyopasuka, pikipiki na gari jingine likiwa na bumper iliyovunjika.

Mama huyo alipokuwa akisimulia mkasa huo mchungu, alieleza kwamba wanne hao walimwambia walikuwa sawa mara ya mwisho alipozungumza nao.

"Mara ya mwisho nilizungumza nao mida ya saa 9.30 waliniambia wako sawa. George aliondoka saa 9 kwenda kumchukua dada yake sikudhani hatarudi. Sijui waliendaje wote na alihusika," alisema.