Bajeti: Mahakama yapata Shilingi bilioni 5 za ziada

Hili ni ongezeko kutoka Shilingi bilioni 18.8 katika mwaka wa kifedha 2022/2023 hadi Shilingi bilioni 23.

Muhtasari

• Kiasi hicho kilitangazwa na Waziri wa Hazina Njuguna Ndung' u siku ya Alhamisi mnamo alasiri alipokuwa akisoma makadirio ya Bajeti ya 2023-24.

•Tangu aingie madarakani mwaka jana, serikali ya Kenya Kwanza ilikuwa imeahidi kuongeza bajeti ya mwaka ya Mahakama kwa Shilingi bilioni 3 kila mwaka.

Bajeti: Mahakama yapata Shilingi bilioni 5 za ziada
Bajeti: Mahakama yapata Shilingi bilioni 5 za ziada

Mahakama inatazamiwa kuongezwa kwa bajeti baada ya serikali kutenga Shilingi bilioni 5 za ziada katika mwaka wa kifedha wa 2023/2024.

Hili ni ongezeko kutoka Shilingi bilioni 18.8  katika mwaka wa kifedha 2022/2023 hadi Shilingi bilioni 23.

Kiasi hicho kilitangazwa na Waziri wa Hazina Njuguna Ndung' u siku ya Alhamisi mnamo alasiri alipokuwa akisoma makadirio ya Bajeti ya 2023-24.

Tangu aingie madarakani mwaka jana, serikali ya Kenya Kwanza ilikuwa imeahidi kuongeza bajeti ya mwaka ya Mahakama kwa Shilingi bilioni 3 kila mwaka.

Rais William Ruto alisema bajeti hiyo itasaidia kujenga miundo msingi inayohitajika.

"Tumejitolea kuongeza (bajeti) kwa Sh3 bilioni ili kuhakikisha pia tunaajiri idadi inayohitajika ya wafanyakazi na kujenga vifaa vya ICT ili Mahakama yetu iweze kutekeleza majukumu yake," alisema awali.

Ripoti ya Mwaka ya Idara ya Mahakama 2022 ilikuwa imetaja uhaba wa fedha kuwa mojawapo ya changamoto.

Katika mapendekezo yake, ripoti hiyo ilisema bunge linapaswa kurekebisha sheria (Sheria ya PFM) ili kudhamini Mahakama angalau asilimia 2.5 ya bajeti ya kitaifa ili kulinda uhuru wa kifedha wa Mahakama kama inavyotajwa katika Katiba.

"Ufadhili wa ziada utasaidia kuajiri majaji, maafisa wa mahakama na kada muhimu za wafanyikazi wa mahakama ili kuongeza rasilimali kufikia angalau asilimia 80 ya kazi iliyoidhinishwa," Ruto alisema.

Baadhi ya fedha hizo pia zitalenga kutekeleza masharti na ya huduma yaliyorekebishwa kwa maafisa wa mahakama, kukagua masharti ya huduma ya wafanyikazi wa mahakama na pia uanzishaji na ujenzi wa mahakama katika kaunti na kaunti ndogo.

Imetafsiriwa na: HALIMA ASAFA