Mamlaka ya kusimamia vyakula na dawa, FDA imebaini bangi haina madhara kwa afya

Utafiti huo wa FDA, kamili kwa Kiingereza kama Food and Drug Administration, pia ulionyesha kuwa bangi ina kiwango cha chini kusababisha uzoefu kwa watumiaji wake.

Muhtasari

• Watafiti hao wanataka bangi iwekwe katika Kitengo cha Tatu kinachosheheni uzoefu wa wastani hadi wa chini kimwili na kisaikolojia, ripoti hiyo ilisema.

• FDA ni shirika lililoko chini ya Wizara ya Afya na Huduma kwa Binadamu, nchini Marekani.

Mamlaka inayosimamia vyakula na dawa humu nchini, FDA imebaini kwamba vangi haina madhara makubwa kwa afya ya binadamu, kinyume na ilivyodhaniwa hapo awali.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Taifa Leo, utafiti ulifanywa na wanasayansi kutoka FDA na kubaini kwamba bangi ina uwezo wa chini kutumiwa vibaya ikilinganishwa na dawa zingine za kulevya kama vile heroni.

Utafiti huo wa FDA, kamili kwa Kiingereza kama Food and Drug Administration, pia ulionyesha kuwa bangi ina kiwango cha chini kusababisha uzoefu kwa watumiaji wake.

FDA ni shirika lililoko chini ya Wizara ya Afya na Huduma kwa Binadamu, nchini Marekani.

Kwa sasa bangi imeorodheshwa kama dawa ya Kitengo cha Kwanza kinachosheheni dawa zenye kiwango cha juu zaidi cha kutumiwa vibaya na uwezo wa kusababisha watumiaji wake kushindwa kujitegemea kisaikolojia, au kimwili.

Watafiti hao wanataka bangi iwekwe katika Kitengo cha Tatu kinachosheheni uzoefu wa wastani hadi wa chini kimwili na kisaikolojia, ripoti hiyo ilisema.

Nchini Kenya, bangi ni miongoni mwa dawa za kulevya zilizopigwa marufuku; kupandwa, kuuzwa na kutumika, licha ya juhudi za aliyekuwa mgombea urais George Wajackoyah kutaka mmea huo kuhalalishwa.

 Katika manifesto yake kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022 Agosti, wakili huyo msomi, George Wajackoyah aliyekuwa akitumia mmea wa bangi kama nembo ya chama chake, alikuwa akipigia debe kuhalalishwa kwa ukulima wa bangi si tu kwa ajili ya matumizi ya humu nchini bali pia kibiashara, akisema kwamba bangi ina thamani ya juu ambayo kuuzwa kwake katika mataifa ya nje kungeliingizia taifa faida kubwa na hivyo kuikomboa nchi kutoka kwa minyororo ya mikopo ya kigeni.

Kwa bahati mbaya, ndoto hiyo ilididimia baada ya Wajackoyah kushindwa kaitka kinyang’anyiro hicho ambapo alimaliza kwa mbali kaitka nafasi ya tatu kwa kujizolea takribani kura elfu 50 pekee.