Mackenzie na wenzake wasinzia mahakamani wakisomewa mashtaka kwa saa 2

Wote walitarajiwa kukiri hatia au kutokuwa na hatia kwa kila makosa 238. Ilikuwa imekubaliwa kwamba wanakiri hatia au hawana hatia kwa pamoja kama kwaya.

Muhtasari

• Wote walitarajiwa kukiri hatia au kutokuwa na hatia kwa kila makosa 238.

• Ilikuwa imekubaliwa kwamba wanakiri hatia au hawana hatia kwa pamoja kama kwaya.

Mhubiri Machenzi na wenzake mahakamani.
Mhubiri Machenzi na wenzake mahakamani.
Image: CHARLES MGHENYI// THE STAR

Mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie na washtakiwa wenzake wengine 94 walilazimika kusubiri kwa zaidi ya saa mbili huku mahakama ikiwasomea mashtaka 238 ya kuua bila kukusudia.

Karatasi ya mashtaka ilikuwa na kurasa 479.

Mashitaka yanayowakabili washtakiwa 95 yalianza kusomewa majira ya saa 1:54 usiku, lakini hadi saa 15:30 jioni makarani wa mahakama hiyo walikuwa wameshughulikia makosa 100 pekee.

Mawakili wa upande wa mashtaka walilalamika kuwa baadhi ya washukiwa walikuwa wamesinzia wakati mashtaka yakiendelea kusomwa.

Wote walitarajiwa kukiri hatia au kutokuwa na hatia kwa kila makosa 238.

Ilikuwa imekubaliwa kwamba wanakiri hatia au hawana hatia kwa pamoja kama kwaya.

"Tumebaini kuwa baadhi ya washtakiwa hawakubaliani na mashtaka. Kwa rekodi ya mahakama, wote wanapaswa kuwa wasikivu na kujibu," mmoja wa mawakili wa upande wa mashtaka alisema.

Hakimu Mkuu wa Mombasa Alex Ithuka aliwataka washukiwa wote kuwa macho.

Kikao cha mahakama kilipangwa kufanyika saa 9:30 alfajiri, lakini kilichelewa baada ya washukiwa hao kufika mahakamani saa sita mchana.

Kulingana na wasimamizi wa magereza basi la Magereza lililokuwa limewabeba washukiwa hao kutoka Gereza la Shimo La Tewa hadi Mahakama ya Sheria ya Mombasa liliharibika katika eneo la Bombolulu.

"Makanika walijaribu kukarabati basi kwa karibu saa moja. Lori ilibidi kuletwa kubeba washukiwa," afisa mmoja alisema.

Lori hilo pia lilipata tatizo la kimitambo katika eneo la Bondeni ndani ya mji wa Mombasa.

Gari la polisi aina ya Landcruiser lilibidi kuletwa kusaidia kuwahamisha washukiwa wote katika Mahakama ya Sheria ya Mombasa katika vikundi vidogo.

Washukiwa hao 95 wanakabiliwa na mashtaka 238 ya kuua watu ambao miili yao iliopolewa kutoka Shakahola.

Wiki iliyopita, 95 hao pia walishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na ugaidi kwa vifo vya watu waliofukuliwa kutoka Shakahola.

Wote walikana mashtaka.