Mahakama yaamuru Mackenzie, wengine 30 kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kesi ya mauaji

Takriban watoto 238 walikuwa miongoni mwa miili 429 ya watu iliyotolewa katika msitu mkubwa wa Shakahola.

Muhtasari

• Baada ya uchunguzi wa miezi tisa, Mkurugenzi wa Mashtaka alisema Mackenzie na wengine 30 walihusika na vifo vya watu hao ,wengi wao wakiwa watoto.

Mhubiri Paul Mackenzie na baadhi ya wafuasi wa kanisa lake wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji.
Mhubiri Paul Mackenzie na baadhi ya wafuasi wa kanisa lake wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji.
Image: BBC

Mahakama kuu mjini Malindi imeupa upande wa mashtaka siku 14 kufanya tathmini ya afya ya akili kwa Paul Mackenzie na washtakiwa wengine 30 kabla ya kusomewa mashtaka kwa madai ya mauaji ya watu wengi huko Kilifi.

Takriban watoto 238 walikuwa miongoni mwa miili 429 ya watu iliyotolewa katika msitu mkubwa wa Shakahola.

Walikufa baada ya kudaiwa kulazimishwa kufunga kwa wiki.

Kuna madai kwamba baadhi ya waathiriwa walinyongwa hadi kufa.

Baada ya uchunguzi wa miezi tisa, Mkurugenzi wa Mashtaka alisema Mackenzie na wengine 30 walihusika na vifo vya watu hao ,wengi wao wakiwa watoto.

Mackenzie na washtakiwa wenzake walifikishwa mahakamani Jumatano, lakini DPP aliomba wiki mbili kufanya uchunguzi wa kiakili kabla ya kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Timu ya utetezi ikiongozwa na Wycliff Makasembo ilipinga maombi hayo.