Baraza la Ulinzi lafanya mkutano wa dharura baada ya ajali ya chopper

Awali polisi walisema maafisa watano walifariki na watatu walinusurika.

Muhtasari
  • Wajumbe wengine ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, makamanda watatu wa vikosi vya ulinzi na Katibu Mkuu katika Wizara inayohusika na ulinzi.
Mbunge wa Garissa Aden Duale
Mbunge wa Garissa Aden Duale
Image: MAKTABA

Baraza la Ulinzi kwa sasa liko katika mkutano wa dharura baada ya chopa ya KDF kuanguka Kaben, Marakwet Mashariki.

Vyanzo vya habari vilieleza kuwa kikao hicho kiliitishwa ili kutathmini hali ilivyokuwa kufuatia ajali hiyo ya chopa na kutoa taarifa kwa nchi.

Baraza hilo linaongozwa na Waziri wa Ulinzi.

Hata hivyo, Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi si mjumbe wa Baraza.

Wajumbe wengine ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, makamanda watatu wa vikosi vya ulinzi na Katibu Mkuu katika Wizara inayohusika na ulinzi.

Baraza linawajibika kwa sera ya jumla, udhibiti na usimamizi wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya; na hutekeleza majukumu mengine yoyote yaliyowekwa na kitaifa

Baraza la Ulinzi ndilo chombo cha juu zaidi cha kufanya maamuzi kinachohusika katika uendeshaji wa kila siku wa Jeshi la Ulinzi la Kenya.

Baraza la Ulinzi linahusika na operesheni na mikakati ya muda mfupi na mrefu ya Jeshi la Ulinzi la Kenya.

Baraza la Ulinzi litaweka sera na kusimamia vipengele vya utendaji vya kila siku vya Jeshi la Ulinzi la Kenya.

Pia wanawajibika kwa sera ya jumla, udhibiti na usimamizi wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya.

Baraza hutekeleza majukumu mengine yoyote yaliyowekwa na sheria ya kitaifa.

Chopa hiyo inasemekana ilikuwa imebeba watu 12 wakiwemo maafisa wa cheo cha Jenerali iliposhuka.

Walioshuhudia walisema kuwa iliwaka moto wakati wa kuanguka.

Kulikuwa na mtu mmoja tu aliyenusurika anayeaminika kuwa mpiga picha, maafisa wengine walisema.

Eneo hilo lilizingirwa mara baada ya tukio hilo.

Maafisa hao walikuwa wakichunguza eneo hilo kabla ya mipango ya kutumwa kwa wanajeshi zaidi ili kupambana na wezi wa mifugo.

Awali polisi walisema maafisa watano walifariki na watatu walinusurika.