Raila Odinga aomboleza kifo cha Jenerali Francis Ogolla

“Siku mbaya kwa Kenya: Mke wangu Ida na mimi tumehuzunishwa sana na kifo cha Jenerali Francis Ogolla, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi."

Muhtasari
  • Jenerali Ogolla, pamoja na wanajeshi wengine kumi na moja, walihusika katika ajali mbaya ya helikopta katika eneo la Sindar, eneo la Kaben huko Elgeyo Marakwet, ambayo ilileta taharuki kote nchini
Jenerali Francis Ogolla na Rila Odinga
Image: Hisani

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Jenerali Francis Omondi Ogolla, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, aliyepoteza maisha katika ajali ya helikopta.

Jenerali Ogolla, pamoja na wanajeshi wengine kumi na moja, walihusika katika ajali mbaya ya helikopta katika eneo la Sindar, eneo la Kaben huko Elgeyo Marakwet, ambayo ilileta taharuki kote nchini.

Katikaheshima yake kwa Jenerali Ogolla, Raila Odinga alisema: “Siku mbaya kwa Kenya: Mke wangu Ida na mimi tumehuzunishwa sana na kifo cha Jenerali Francis Ogolla, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi."

Akiongeza, “Tunaungana na taifa katika kuomboleza kifo chake. Jenerali Ogolla alikuwa mzalendo wa kweli, mwanajeshi aliyepambwa sana na mtaalamu aliyekamilika ambaye alitumikia nchi yetu kwa kujitolea bila kuyumbayumba.”

Akielezea mshikamano na familia iliyojawa na huzuni, Raila aliongeza: “Mioyo yetu ni kwa familia yake, wafanyakazi wenzake katika KDF na taifa zima tunapoomboleza kifo huu mkubwa. Pia tunatuma rambirambi zetu kwa familia za timu ya KDF iliyoandamana na Jenerali Ogolla. Tunajua kwamba kwa wakati huu, maneno hayatatosha kufariji huzuni zenu kubwa. Tunawaombea Bwana awafariji na roho za wote waliofariki zipate amani ya milele.”

 

Moses Wetangula, Spika wa Bunge la Kitaifa pia aliungana na taifa kuomboleza msiba wa CDF Ogolla.

Katika heshima kubwa, Spika Wetangula alielezea masikitiko yake makubwa kutokana na kufariki kwa Jenerali Ogolla na maafisa wenzake ambao utumishi wao wa kujitolea kwa taifa utakumbukwa kwa taadhima.

“Nasimama pamoja na taifa na vikosi vyetu vilivyo na nidhamu katika kuomboleza msiba wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Francis .O. Ogolla, ambaye alifariki katika ajali ya helikopta akiwa kazini katika Wilaya ya Elgeiyo Marakwet inalemea mioyo yetu,” alisema Spika Wetangula.

Spika Wetangula amewatakia manusura wa ajali hiyo ahueni ya haraka na kuomba dua ili roho za marehemu zipate amani ya milele.