Rais Ruto atangaza Siku 3 za Maombolezo ya Kitaifa kwa CDF Francis Ogolla

Rais Ruto aliagiza bendera zote nchini Kenya zipepee nusu mlingoti katika kipindi cha siku tatu.

Muhtasari

• "Huu ni wakati wa huzuni kubwa kwangu, kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya. Nchi yetu imepoteza mmoja wa majenerali wake shupavu, maofisa shupavu," Ruto alisema.

Rais Ruto kuongeza idadi ya watoza ushuru kwenye masoko, mitaa.
Rais Ruto kuongeza idadi ya watoza ushuru kwenye masoko, mitaa.
Image: Facebook

Rais William Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Francis Omondi Ogolla aliyefariki katika ajali ya helikopta siku ya Alhamisi eneo la Sindar kaunti ya Elgeyo Marakwet, pamoja na wanajeshi wengine tisa.

Akitangaza rasmi kifo cha Ogolla Ruto aliomboleza marehemu kama afisa shupavu wa kijeshi na mzalendo wa kweli aliyejitolea maisha yake kutumikia nchi yake kwa heshima na upendeleo usio na kifani.

"Huu ni wakati wa huzuni kubwa kwangu, kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya. Nchi yetu imepoteza mmoja wa majenerali wake shupavu, maofisa shupavu," Ruto alisema.

Akitoa risala za rambirambi kwa familia na marafiki wa Ogolla, rais aliagiza bendera zote nchini Kenya zipepee nusu mlingoti katika kipindi cha siku tatu.

"Kwa heshima ya maisha na taaluma ya kijeshi ya Jenerali ambaye alipoteza maisha sio tu akiwa ofisini bali katika majukumu ya kijeshi, taifa litaadhimisha muda wa siku tatu za maombolezo kuanzia Aprili 19," Rais alisema.