Rais William Ruto aitisha kikao cha dharura cha baraza la kitaifa la usalama

Mkutano huu unajiri wakati imeriptiwa kuwa ndege ya kijeshi imeanguka katika eneo la Elgeyo Marakwet.

Muhtasari

• Helikopta ya Kenya Air Force Huey ilikuwa imetoka katika shule ya msingi ya eneo hilo ilipoanguka na kuwaka moto. 

Rais William Ruto aidhinisha Mswada wa Fedha wa 2023 Ikulu Juni 26, 2023.
Rais William Ruto aidhinisha Mswada wa Fedha wa 2023 Ikulu Juni 26, 2023.
Image: PCS

Rais William Ruto ameitisha mktutano wa dharura wa baraza kuu la kitaifa la usalama.

Mkutano huu unajiri wakati imeriptiwa kuwa ndege ya kijeshi imeanguka katika eneo la Elgeyo Marakwet. 

Kulingana na taarifa ni kwamba ndege hiyo ilikuwa imebeba maafisa wakuu wa jeshi. 

Helikopta ya Kenya Air Force Huey ilikuwa imetoka katika shule ya msingi ya eneo hilo ilipoanguka na kuwaka moto. 

Makao makuu ya Idara ya Ulinzi ilisema taarifa itatolewa kuhusu tukio hilo. Chopa hiyo inasemekana ilikuwa imebeba watu 12 wakiwemo maafisa wa cheo cha Jenerali ilipoanguka. 

Walioshuhudia walisema kuwa iliwaka moto wakati wa kuanguka. Kulikuwa na mtu mmoja tu aliyenusurika anayeaminika kuwa mpiga picha, maafisa wengine walisema. Eneo hilo lilizingirwa mara baada ya tukio hilo. 

Maafisa hao walikuwa wakichunguza eneo hilo kabla ya mipango ya kutumwa kwa wanajeshi zaidi ili kupambana na wezi wa mifugo. 

Awali polisi walisema maafisa watano walifariki na watatu walinusurika.