Maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa umeme Jumatatu- KPLC

KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Aprili 22.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tatu yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Aprili 22.

Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nyamira, na Homabay. 

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za eneo la Parklands zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Mogeni na Sanganyi katika kaunti ya Nyamira zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tano asubuhi.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Asumbi, Rangwe na Nyawita katika kaunti ya Homabay pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.