KPLC yatangaza kaunti 8 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme Jumatano

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Aprili 24

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Eneo la Chuo Kikuu cha Moi katika kaunti ya Uasin Gishu litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Aprili 24.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Uasin Gishu,Busia,Kisii, Migori, Homabay, Nyeri,  na Kiambu.

Katika kaunti ya Nairobi, mtaa wa Garden Estate utaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Chuo Kikuu cha Moi katika kaunti ya Uasin Gishu litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Busia, baadhi ya sehemu za maeneo ya Mundika, Nasewa, na Lung'a zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Nyangena na Nyabururu katika kaunti ya Kisii zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa nane alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Uriri, Kakrao na God Jope katika kaunti ya Migori zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Ramula, Mawego, na Ramba katika kaunti ya Homabay pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Nyeri, baadhi ya sehemu za maeneo ya Blueline, Munyu na Kimahuri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za maeneo ya Ruaka, na Mulberry katika kaunti ya Kiambu oia zitakosa umeme .