Tofauti kati ya Muguka na Miraa

Ripoti ya NACADA imefichua kuwa idadi kubwa ya Wakenya wametumia Miraa angalau mara moja katika maisha yao hii ikiwa ni asilimia 55 ikilinganishwa na Muguka,asilimia 31

Muhtasari

•Kaunti za Mombasa na Kilifi zilipiga marufuku uuzaji na usambazaji wa muguka wiki jana, na hivyo kuashiria hatua kubwa katika juhudi za eneo la pwani kuzuia usambazaji na matumizi ya kichocheo hicho.

•Kwenye kikao kati ya Rais Ruto na waziri wa kilimo,Mithika Linturi ,Jumatatu 27,2024 Muguka umetambuliwa na sheria za kitaifa, sheria au amri nyingine zozote zinazokinzana na sheria za kitaifa ni batili.

Miraa
Image: maktaba

Baadhi ya viongozi katika kaunti ya Mombasa,Kilifi na Taita Taveta wamekuwa mstari mbele kukomesha matumizi ya muguka maeneo ya Pwani..

Muguka na miraa ni mimea ambayo majani yake mbichi na matawi laini hutafunwa ili kutoa juisi ambayo hubadilisha hali ya mtumiaji. Miraa ina shina nyororo yenye majimaji ambayo hutafunwa, Muguka ni kichaka kifupi kiasi chenye majani ya kuliwa na yasiyo na shina.

Muguka huzalishwa katika kaunti ya Embu huku miraa hukuzwa zaidi katika kaunti ya Meru. Muguka inachukuliwa kuwa bidhaa ya bei nafuu ikilinganishwa na miraa na hivyo inapatikana kwa urahisi (Muguka) kwa watumiaji.

Utafiti uliofanywa na mamlaka ya kitaifa ya kampeni dhidi ya unywaji pombe na madawa ya kulevya (NACADA) ulifichua kuwa idadi kubwa ya Wakenya wametumia miraa angalau mara moja katika maisha yao (asilimia 55) ikilinganishwa na muguka (asilimia 31).

Madhara ya kutafuna muguka kulingana na ripoti ya NACADA, husababisha athari za kijamii na kiafya ikiwa ni pamoja na utumbo, na athari za akili. Muguka ina nguvu zaidi kuliko miraa kwani inabidi mtu atumie majani mengi ili kuchangamshwa.

Aidha,kutafuna majani ya muguka kunaleta uraibu kidogo kuliko shina la miraa.Kulingana na ripoti ya NACADA, bidhaa zote mbili zina athari zinazofanana ambazo ni pamoja na kukosa usingizi, wasiwasi, msukumo kupita kiasi, kubadilika rangi kwa meno na kuvimba kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kumbukumbu iliyoharibika, kukosa usingizi, kutoona vizuri,kukosa nguvu za kiume pamoja na kizunguzungu.

Kwenye kikao kati ya Rais William Ruto na waziri wa kilimo Mithika Linturi pamoja na gavana wa Embu,Cecily Mbarire Jumatatu 27, Rais alisema kuwa marufuku iliyowekwa dhidi ya muguka katika kaunti za Kilifi na Mombasa ni batili. Rais alisema muguka ni zao lililopangwa kwa mujibu wa sheria ya mazao ya 2013 na kanuni za Miraa 2023. Sheria ya Kanuni za Miraa ilipitishwa na Bunge na Baraza la Magavana kwa pamoja na baraza la magavana.

"Kwa kuwa muguka umetambuliwa na sheria za kitaifa, sheria au amri nyingine zozote zinazokinzana na sheria za kitaifa ni batili," Ruto alisema katika ujumbe wake kutoka Ikulu.