Rais Ruto na naibu wake Gachagua wafanyiwa maombi katika kanisa ya Akorino, Nakuru

Ikumbukwe wengi wamekuwa wakiitaka kanisa kuingilia kati kama kuna kutoelewana baina ya viongozi hao wawili ambao wamekuwa wakionekana kusoma kutoka kurasa mbili tofauti kuhusu ugavi wa rasilimali za taifa.

Muhtasari

• Viongozi hao wawili walihudhuria ibada hiyo iliyoandaliwa na kanisa la Akorino, iliyopewa jina la Akorino National Thanksgiving Prayer Conference.

• Waliandamana na umati wa viongozi wengine kutoka kaunti ya Nakuru pamoja na maeneo mengine ya nchi.

• Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi hao wawili kuhudhuria ibada pamoja katika kipindi cha mwezi mmoja.

Image: screengrab//YT

Jumapili asubuhi, rais Ruto na naibu wake Gachagua walikuwa miongoni mwa waumini kadhaa walioudhuria ibada ya maombi ya kitaifa ya dhehebu la Akorino katika kaunti ya Nakuru.

Viongozi hao wawili walihudhuria ibada hiyo iliyoandaliwa na kanisa la Akorino, iliyopewa jina la Akorino National Thanksgiving Prayer Conference.

Waliandamana na umati wa viongozi wengine kutoka kaunti ya Nakuru pamoja na maeneo mengine ya nchi.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi hao wawili kuhudhuria ibada pamoja katika kipindi cha mwezi mmoja.

Katika mkutano huo wa maombi, viongozi wakuu wa Akorino walionekana wakiwawekea mikono ya maombi Gachagua na Ruto ambao walikuwa wameketi na kuinamisha nyuso zao kuheshimu maombi.

Haya pia yanajiri huku kukiwa na mazungumzo ya mtafaruku kati ya Rais Ruto na Gachagua kuhusu ugavi wa mgao.

Wakati DP na viongozi walioshirikiana naye wakitaka mfumo wa mgawanyo wa mapato wa mtu mmoja kwa shilingi moja, rais na viongozi wanaoshirikiana naye wanasisitiza kuwa itakuwa haitendei haki mikoa mingine.

Ingawa, kuna gumzo kuhusu mpasuko, Ruto na Gachagua wamekuwa wakihudhuria shughuli rasmi za serikali pamoja.

Ikumbukwe wengi wamekuwa wakiitaka kanisa kuingilia kati kama kuna kutoelewana baina ya viongozi hao wawili ambao wamekuwa wakionekana kusoma kutoka kurasa mbili tofauti kuhusu ugavi wa rasilimali za taifa.