Asante kwa kutetea Kenya, watu wake - Ruto awaambia polisi

Waandamanaji hao watatu walihofiwa kufariki katika tukio hilo walipokuwa wakikaribia Majengo ya Bunge. Kundi jingine lilikuwa limeteremsha lango karibu na Seneti.

Muhtasari

• Takriban waandamanaji watatu waliripotiwa kupigwa risasi nje ya Majengo ya Bunge huku kundi la watu wakipambana na polisi.

Rais William Ruto
Rais William Ruto
Image: PCS

Rais William Ruto amepongeza vyombo vya usalama vya serikali kwa kulinda Kenya na watu wake wakati wa maandamano ya Jumanne ya kupinga Mswada wa Fedha.

“Ninawashukuru maafisa wetu wa usalama ambao walikuwa kazini leo kwa kujituma kadiri wawezavyo, katika kulinda Kenya na watu wake,” Ruto alisema.

Mkuu huyo wa Nchi alizidi kuwahakikishia Wakenya kuhusu usalama zaidi akisema "ameagiza vyombo vyote vya usalama wa taifa kupeleka hatua zote za kuzuia majaribio yoyote ya wahalifu hatari kuhujumu usalama na uthabiti wa nchi."

"Ninahakikishia taifa, kwamba Serikali imekusanya rasilimali zote zinazotolewa na taifa ili kuhakikisha kuwa hali ya aina hii, haitajirudia tena, kwa gharama yoyote," Ruto alisema.

"Watu wa Kenya wanapolala usiku huu, ninawapa hakikisho langu kwamba usalama wenu, wa familia na mali zenu, unasalia kuwa kipaumbele changu kikuu."

Maandamano hayo ya Jumanne yaliripotiwa kusababisha vifo vya watu 10 baada ya kudaiwa kupigwa risasi na polisi wa kupambana na ghasia.

Takriban waandamanaji watatu waliripotiwa kupigwa risasi nje ya Majengo ya Bunge huku kundi la watu wakipambana na polisi.

Kundi hilo lilikuwa likipinga Mswada wa Fedha. Takriban wengine wanne walijeruhiwa na kuchukuliwa na ambulensi, mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei alisema.

Waandamanaji hao watatu walihofiwa kufariki katika tukio hilo walipokuwa wakikaribia Majengo ya Bunge. Kundi jingine lilikuwa limeteremsha lango karibu na Seneti.

Lori la polisi liliteketezwa nje ya bunge. Wabunge walihamishwa huku kundi hilo likikabiliana na polisi.