Rais Ruto atupilia mbali mswada wa fedha 2024/25

Rais Ruto alisema kwamba hatua yake imetokana na maoni ya wakenya.

Muhtasari

• Mswada huo ulipitishwa na bunge na kuwasilishwa kwa rais ili kutiwa saini.

RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais William Ruto ametupilia mbali mswada wa fedha wa mwaka 2024/25.

Akihutubia taifa siku ya Jumatano rais alisema kwamba hatua yake imetokana na maoni ya wakenya.

Rais alikiri kuwa wakenya wengi walionekana kuupinga mswada huo na licha ya kuwa serikali ilikuwa na mipango kupata pesa zaidi za maendeleo itabidi atafute njia mbadala.

Baadhi ya mapendekezo ya kodi ambayo awali yaliletwa katika muswada huo ni pamoja na asilimia 16 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mkate, Ushuru wa Bidhaa kwenye mafuta ya mboga, VAT kwenye usafirishaji wa sukari, asilimia 2.5 ya Ushuru wa Magari na Ushuru wa mazingira kwa bidhaa zinazotengenezwa nchini.

Mswada huo ulipitishwa na bunge na kuwasilishwa kwa rais ili kutiwa saini.