KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumatatu

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya JumatATU, Julai 1.

Muhtasari

•Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Julai 1. 

Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Kiambu na Bomet.

Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kiambururu, Kanjai, Thindigua, na Njathaini zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kapkoros na Kiplokyi katika kaunti ya Bomet pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.