Majambazi wamlawiti mwanaume kisha kukata sehemu zake za siri Kiambu

Taarifa ya polisi ilibainisha kuwa mwanamume huyo ni mlemavu.

Muhtasari

• Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 48 anaripotiwa kulawitiwa na majambazi hao kisha kukatwa sehemu zake za siri.

• Mwanamume huyo anapokea matibabu katika hospitali ya Kiambu Level Five.

Wataalam wa upasuaji katika chumba cha upasuaji wakimshughulikia mgonjwa
Wataalam wa upasuaji katika chumba cha upasuaji wakimshughulikia mgonjwa
Image: MAKTABA

Hali tete na ya wasiwasi iilijitokeza katrika eneo la Ndeiya kaunti ya Kiambu baada ya mwanamume mmoja kudhulumiwa kingono na genge lisilojulikana.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 48 anaripotiwa kulawitiwa na majambazi hao kisha kukatwa sehemu zake za siri. Tukio hilo lilimwacha akivunja damu nyingi nusura kufariki, kabla ya kukimbizwa hospitalini.

Wasamaria wema walimkimbiza  katika hospitali ya Kiambu Level 5 baada ya kumwona akiwa amelala katika hali mahututi huku nguo zake zikiwa zimeararuriwa. 

Mmoja wa waliomsaidia alisema alimuona mwathiriwa akiwa katika hali mbaya na mavazi yake yakiwa yamelowa damu.

''Nilipomwona mwanamume huyo tulimpa huduma ya kwanza kabla ya kumfikisha hospitalini. Alikuwa na damu nyingi kwenye mavazi yake,'' alisema.

"Tunashuku kuwa kinywaji cha mwathiriwa kilikuwa na dawa za kulevya. Ni lazima washukiwa walitumia dawa kama hiyo kabla ya kumwandama njiani. Inasikitisha!," mkazi mwingine alisema.

Wakazi wametoa wito kwa idara ya polisi kuchukua hatua ya haraka ili kuhakikisha waliotekeleza kitendo hicho wamekamatwa.

Taarifa ya polisi iliyotolewa na Roseline Mnyolmo ilisema uchunguzi unaendelea kufanyika ili kuhakikisha waliotekeleza unyama huo wametiwa mbaroni na kukabiliana na sheria.

Taarifa ya polisi ilibainisha kuwa mwanamume huyo ni mlemavu.