Maseneta wa Azimio wapuuzilia mbali mgawanyiko kwenye muungano huo

"Tumeshauriana sisi wenyewe na wakuu wetu na sisi ni wamoja na hakuna migawanyiko hata kidogo

Muhtasari
  • Akizungumza katika majengo ya bunge siku ya Jumatatu, Seneta wa Narok Ledama Olekina alifafanua kuwa muungano huo ungali imara
Maseneta wa Azimio yapuuzilia mbali mgawanyiko kwenye muungano huo

Maseneta wanaohusishwa na muungano wa Azimio la Umoja wamepuuzilia mbali ripoti kuwa kuna mgawanyiko ndani ya muungano huo kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Akizungumza katika majengo ya bunge siku ya Jumatatu, Seneta wa Narok Ledama Olekina alifafanua kuwa muungano huo ungali imara.

Olekina, ambaye aliongoza timu hiyo, alidai kuwa walifanya kikao Jumatatu asubuhi na vinara wa muungano huo Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Uhuru Kenyatta na kuwahakikishia kuwa hakuna tofauti kati ya viongozi katika Azimio katika Seneti.

Viongozi wengine kutoka Azimio akiwemo Kiongozi wa Wachache katika Seneti Stewart Madzayo, Fatuma Dhulloh na Enock Wambua waliongeza kuwa muungano huo utasalia sawa na kwamba madai yanayoripotiwa ni ya uongo.

"Tumeshauriana sisi wenyewe na wakuu wetu na sisi ni wamoja na hakuna migawanyiko hata kidogo na hakuna kinachopaswa kusababisha hofu

Tulikutana na Raila, Uhuru na Kalonzo Musyoka asubuhi ya leo. Kuna sauti moja tu ambayo itazungumza azimio katika Seneti, hakuna mtu mwingine,” alisema Madzayo.