"Tuko serikalini na hatuwezi zungumza mengi kuhusu sisi wenyewe - Havi atetea ukimya wake

Wakili Havi alikuwa mwenye mazoea ya kusema sana kuhusu masuala ya utawala wa kisheria.

Muhtasari

• “Wakili mmoja aliniuliza leo, “Mheshimiwa Rais, siku hizi uko kimya sana. Husemi chochote kuhusu masuala ya utawala wa sheria.” - Havi

Wakili Havi atetea ukimya wake siku za hivi karibuni
Wakili Havi atetea ukimya wake siku za hivi karibuni
Image: Facebook

Aliyekuwa rais wa chama cha wanasheria nchini LSK Nelson Havi amekuwa mkimya tangu kupoteza azma yake ya kutaka kuwa mbunge wa Westalands.

Havi ambaye alikuwa akiwania kwa mara yake ya kwanza kupitia chama cha UDA alishindwa na mbunge Timothy Wanyonyi wa ODM ambaye alikuwa anakitetea kiti hicho kwa mara ya tatu mtawalia.

Baada ya kupoteza, Havi ambaye alikuwa anajulikana sana kupasha serikali haswa kipindi akihudumu kama rais wa LSK alikuja akakimya ghafla.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, wakili Havi amefunguka kuhusu kimya chake na katika hali ya utani, alisema kwamba mtu ukiwa ndani ya serikali huna haja ya kubweka sana.

Alidokeza kwamab alikutana na mtu ambaye alimuuliza swali hilo na akamjibu kwamba kwa vile William Ruto amabye ni mwandani wake wa karibu ameshaichukua serikali, sasa wamo ndani na hawana haja tena ya kuzungumza sana.

“Wakili mmoja aliniuliza leo, “Mheshimiwa Rais, siku hizi uko kimya sana. Husemi chochote kuhusu masuala ya utawala wa sheria.” "Nilisema mengi juu ya hilo hapo awali. Sasa tuko Serikalini na hatuwezi kuzungumza mengi kuhusu sisi wenyewe”, nilimwambia. Alicheka na kusema, "Tumekukosa huko LSK." Hali alinukuu mazungumzo yake na wakili mwenzake.