Winnie Odinga avunja kimya baada ya kushambuliwa Twitter

Katika taarifa yake Jumatano, Winnie alijitetea dhidi ya shutuma kwamba alihujumu timu ya Azimio

Muhtasari
  • Haya yanajiri saa chhache baada ya msemaji wa Azimio Makau Mutua Katika taarifa  alisema Winnie ni mwanasiasa mchanga na anafaa kuelimishwa
Winnie Odinga
Winnie Odinga

Winnie Odinga amevunja kimya na kusema hakuna binadamu anayestahili kumhukumu.

Katika taarifa yake Jumatano, Winnie alijitetea dhidi ya shutuma kwamba alihujumu timu ya Azimio la Umoja wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

"Yule ambaye amejichanganya katika msukosuko wa wajibu ambao wajasiri hustahimili, lazima atakuwa amefanya maadui. Ikiwa huna, kazi ambayo umefanya ni ndogo. Hujawahi kugeuza kosa kuwa sawa. Umekuwa mwoga katika vita."

Charles Mackay

Ni Mungu pekee ndiye anayeujua moyo wangu, atanihukumu tu,"Winnie Aliandika.

 

Haya yanajiri saa chhache baada ya msemaji wa Azimio Makau Mutua Katika taarifa  alisema Winnie ni mwanasiasa mchanga na anafaa kuelimishwa.

"Wale ambao wamekuwa wakimshambulia Winnie Odinga wakome na waache. Yeye ni mwanamke mchanga katika siasa. Mwanamume amabye yuko kwenye hali yake hatakuwa mjanja sana. Winnie alipata talanta, lakini ushauri utakuwa muhimu. Tuwaunge mkono vijana wetu," Mutua alisema.

Winnie alirejea kwenye mitandao ya Twitter baada ya mwezi mmoja wa kuzima mtandao huo.