Seneta Cherargei:Kupungua kwa bei ya mafuta hakutaonekana mara moja

Bei ya mafuta nchini Kenya ilipanda zaidi mnamo Septemba baada ya serikali mpya kupunguza ruzuku.

Muhtasari
  • Katika hali hii, inamaanisha watumiaji wa dizeli watalipa bei ya juu ili kuhakikisha watumiaji wa petroli wana bei ya chini
Seneta wa Nandi Samson Cherargei
Image: EZEKIEL AMING'A

Seneta wa Nandi Samson Cherargei amesema kwamba kupunguza bei ya mafuta hakutaonekana mara moja kwa sababu ya shilingi dhaifu dhidi ya dola.

Hii ni baada ya Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli mnamo Jumatatu kupunguza bei ya mafuta kwa Sh1 katika ukaguzi wake wa hivi punde wa bei huku ruzuku ikihifadhiwa kwa mafuta taa.

"Kupungua kwa bei ya mafuta hakutaonekana mara moja kwa sababu ya shilingi dhaifu dhidi ya dola licha ya kupungua kwa bei ya mafuta duniani kwa asilimia 30 na madhara ya baada ya Uhuru," Cherargei alisema Jumanne.

Bei ya mafuta nchini Kenya ilipanda zaidi mnamo Septemba baada ya serikali mpya kupunguza ruzuku.

Katika uhakiki wa hivi punde wa EPRA, lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh177.30 jijini Nairobi huku lita ya dizeli ikiuzwa kwa Sh162.00.

Mdhibiti wa nishati alisema bei ya dizeli imetolewa kwa ruzuku na ile ya petroli ya super.

Katika hali hii, inamaanisha watumiaji wa dizeli watalipa bei ya juu ili kuhakikisha watumiaji wa petroli wana bei ya chini.

Cherargei aliongeza kuwa;

"Suluhisho ni kuhakikisha utafutaji wa mafuta wa Tullow Turkana unawezekana kibiashara ili kutumika nchini."