Sabina Chege na Kanini Kega walikuwa wamepotea tutawarudisha nyumbani-Gachagua

Binti wa mbunge huyo mwenye umri wa miaka 10, Natasha Makena, alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Muhtasari
  • Gachagua alizungumza Ijumaa wakati wa ibada ya mazishi ya bintiye mbunge wa Chuka Igamba-Ng'ombe Patrick Munene huko Chuka, kaunti ya Tharaka Nithi
Gachagua asema Uhuru hatimaye umefika
Gachagua asema Uhuru hatimaye umefika
Image: Facebook

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewaomba na kuwasihi viongozi wa upinzani kutoka mlima Kenya kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza.

Gachagua alimtaja aliyekuwa Mbunge wa Kieni Kanini Kega na Mbunge mteule wa Jubilee Sabina Chege ambaye alisema watavutia Kenya Kwanza hatua kwa hatua.

"Tunawashauri viongozi wetu vijana na tunawatayarisha kwa uongozi na kwa mambo makubwa mbeleni kwa sababu hii ni rasilimali yetu na ni jukumu letu kuwatayarisha," Gachagua alisema.

Naibu Rais  alisema, ni kuhakikisha kuwa Kenya ya Kati haipatikani tena ikiwa imegawanyika wakati wa uchaguzi wa kisiasa yajao.

"Hata hii Sabina Chege mtu wa Jubilee tutaweka mbolea akuje sawa,"

Gachagua alizungumza Ijumaa wakati wa ibada ya mazishi ya bintiye mbunge wa Chuka Igamba-Ng'ombe Patrick Munene huko Chuka, kaunti ya Tharaka Nithi.

Binti wa mbunge huyo mwenye umri wa miaka 10, Natasha Makena, alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Naibu Rais alifichua wakati wa ibada ya mazishi kwamba yeye ndiye aliyewashawishi wabunge wa eneo la Mlima Kenya kumpigia kura Kega katika Bunge la Afrika Mashariki.

"Kanini tumeleta jana walikuwa wamepotea, tutaleta kidogo kidogo tunajaribu kurudisha kuwapanga panga mpaka waingie laini," Alizungumza Naibu Rais.