Raila:Nilishinda uchaguzi wa Urais wa Agosti

Raila pia alidai kuwa Ruto anapanga njama ya mapema ya wizi wa kura katika uchaguzi wa 2027.

Muhtasari
  • Rais William Ruto alitangazwa mshindi wa urais lakini Raila ambaye alipinga matokeo katika mahakama ya Juu, alipoteza ombi hilo
Odinga azungumzia Wahindi waliotoweka
Odinga azungumzia Wahindi waliotoweka
Image: Facebook

Kinara wa upinzani Raila Odinga amedai, bila kutoa ushahidi, kwamba alishinda uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Rais William Ruto alitangazwa mshindi wa urais lakini Raila ambaye alipinga matokeo katika mahakama ya Juu, alipoteza ombi hilo.

"Nimekaa nanyi kwa muda mrefu. Mamilioni yenu mlinipigia kura katika uchaguzi uliopita. Tulishinda uchaguzi huo, ukweli utadhihirika, najua hilo," alisema.

"Mamilioni yenu huniita Baba."

Raila pia alidai kuwa idara ya mahakama imetekwa na serikali.

"Mfumo wa haki za jinai unaporomoka. Ndio maana kesi zinafutwa kwa kasi, wahalifu wanasherehekewa na kugeuzwa kuwa mashahidi wa mashtaka," alisema.

Raila pia alidai kuwa Ruto anapanga njama ya mapema ya wizi wa kura katika uchaguzi wa 2027.

Matamshi yake yanakuja baada ya Ruto kuwasimamisha kazi makamishna wanne wa IEBC walioipinga wakiongozwa na naibu mwenyekiti Juliana Cherera.

Katika notisi ya gazeti la serikali siku ya Ijumaa, Rais alisema kusimamishwa kwao kulianza mara moja.

Makamishna wengine ni Justus Nyang’aya, Francis Wanderi na Irene Masit.

Kulingana na Raila, kanuni mpya ya kuteua makamishna wa bodi ya uchaguzi na Bunge siku ya Alhamisi haihusu uadilifu.

"Matukio ya Bunge jana, kuhusu fomula ya kuwateua makamishna wa IEBC na kuwasaka makamishna wanne hayana uhusiano wowote na uadilifu, lakini takriban 2027," alisema.

"Ruto anataka kuvuruga uchaguzi wa 2027. Hatufai kuruhusu hili kutokea.