Raila hatimaye azungumza baada ya Ruto kuwasimamisha makamishna 4 wa IEBC kazi

Mahakama hiyo itaongozwa na Jaji wa Mahakama ya Juu Aggrey Muchelule kama mwenyekiti.

Muhtasari
  • Alikariri kuwa Muungano wa Azimio hautaketi na kuruhusu serikali kuwaondoa makamishna wanne afisini
Odinga azungumzia Wahindi waliotoweka
Odinga azungumzia Wahindi waliotoweka
Image: Facebook

Kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement, Raila Odinga, amejibu hatua ya Rais William Ruto ya kumsimamisha kazi makamu mwenyekiti wa IEBC, Juliana Cherera, na makamishna wengine watatu.

Akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa mashinani wa Nairobi jijini Nairobi mnamo Ijumaa, Disemba 2, Raila alitaja kusimamishwa kazi kama kidikteta na hatua ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Alikariri kuwa Muungano wa Azimio hautaketi na kuruhusu serikali kuwaondoa makamishna wanne afisini.

“Matukio ya Bunge jana kuhusu fomula ya kuwateua makamishna wa IEBC na kuwasaka makamishna wanne hayana uhusiano wowote na uadilifu, lakini kuhusu 2027. Ruto anataka kuvuruga uchaguzi wa 2027. Hatupaswi kuruhusu hili kutokea."

"Mnamo Desemba 7, tutazindua kongamano la mashauriano ya umma katika uwanja wa kihistoria wa Kamkunji. Na tutarejea katika uwanja huo mnamo Desemba 12 ili kuendelea na mashauriano," Raila alisema.

Siku ya Ijumaa, Rais William Ruto aliwasimamisha kazi Makamishna wanne na kuunda mahakama ya kuwachunguza.

Mahakama hiyo itaongozwa na Jaji wa Mahakama ya Juu Aggrey Muchelule kama mwenyekiti.

Ruto pia aliwateua Carolyne Kamende Daudi, Linda Gakii Kiome, Mathew Njaramba Nyabena, Kanali (Mst.) Saeed Khamis Saeed kuwa wanachama wa mahakama hiyo.

Kibet Kirui Emmanuel, Irene Tunta Nchoe wameteuliwa kuwa makatibu wakuu.