Aliyeuwa watoto wake Kisii yuko sawa kiakili kushtakiwa - ripoti ya uchunguzi wa akili

Bw Nelson Ontita sasa atakabiliwa na kesi ya mauaji ya watoto wake wenye umri wa miezi 10 na miaka miwili.

Muhtasari

• Miili ya watoto hao ilipatikana katika shamba la mahindi na mama yao ambaye alitoa tahadhari na kusababisha kukamatwa kwa mume huyo.

Mwanaume aliyeua watoto wake Kisii
Mwanaume aliyeua watoto wake Kisii

Mwanamume aliyedaiwa kuwaua watoto wake wawili katika kijiji cha Kiobegi eneo bunge la Bobasi, Kaunti ya Kisii, yuko sawa kiakili kujibu mashtaka, ripoti ya daktari wa akili inasema.

Bw Nelson Ontita sasa atakabiliwa na kesi ya mauaji ya watoto wake wenye umri wa miezi 10 na miaka miwili.

Mazishi ya watoto hao imefanyika Jumatatu January 16 nyumbani kwao saa chache tu baada ya ripoti ya upasuaji ikisema kuwa watoto hao walifariki kutokana na kuchomwa na chombo chenye ncha kali kwa nguvu.

Mshukiwa alikuwa ameachwa kuwatunza waathiriwa na mkewe alipokuwa akienda kushughulikia kazi zingine.

 Miili ya watoto hao ilipatikana katika shamba la mahindi na mama yao ambaye alitoa tahadhari na kusababisha kukamatwa kwa mume huyo.

 Baada ya kufika mahakamani, upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kutaka ashikiliwe huku tathmini ya kisaikolojia ikifanywa ili kubaini kama alikuwa katika hali nzuri ya kupandishwa kizimbani.

Mwendesha mashtaka-Bw Ian Mukusi aliambia mahakama kwamba maafisa wa uchunguzi walihitaji siku 14 kumzuilia mshukiwa huyo akisubiri kukamilika kwa uchunguzi.

 

Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiakili na ripoti kubaini kuwa mwanaume huyo yuko katika hali nzuri ya kiakili na anaweza kushtakiwa, Kesi hiyo itasikizwa mahakamani Januari 23, 2023.

Mwanzoni mwa mwaka huu visa kadhaa vya kushtusha na kuogofya kama hivyo viliripotiwa kutoka kaunti ya Kisii, watu wakiuana na kuzua taharuki kote nchini.

Mwanaume aliyeua watoto wake Kisii
Mwanaume aliyeua watoto wake Kisii